Mtambo wa Wachina ukinyenyua gari la Kampuni ya Sabena baada ya kupata ajali eneo la maji mazuri Kawetere barabara ya Chunya likiwa linaelekea Tabora leo Asubuhi. |
Wachina wanaojenga barabara ya Chunya wakishangaa gari la Kampuni ya Sabena baada ya kupata ajali eneo la maji mazuri
Kawetere barabara ya Chunya likiwa linaelekea Tabora leo Asubuhi.
Majeruhi wa ajali hiyo Ramadhani Kipese (45) akiwa na majeraha kichwani. |
Kondakta
wa gari la Kampuni ya Sabena Seif Salum (34) akisaidia kuokoa mizigo ya
abiria baada ya kupata ajali eneo la maji mazuri
Kawetere barabara ya Chunya likiwa linaelekea Tabora leo Asubuhi.
Gari la Polisi likiwa eneo la tukio kuokoa mizigo ya majeruhi walolazwa katika Hospital ya Rufaa ya Mbeya.
********************************************
KICHANGA cha Miezi 6 kimefariki
dinia papo hapo na wengine zaidi ya 60 wamenusurika kufa katika ajali mbaya iliyohusisha Basi kampuni
ya Sabena baada ya kuacha njia na kutumbukia katika Mtaro pembezoni mwa Barabara eneo la Maji mazuri Kawetere
nje kidogo ya Jiji la Mbeya.
Kwa mujibu wa Wahanga wa ajali
hiyo iliyotokea jana wamesema imetokana na mwendokasi ambapo Dereva alishindwa
kulimudu basi hilo lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Mwanza.
Wamesema ajali hiyo imetokea
majira ya Saa moja asubuhi ambapo katika
ajali hiyo watu kadhaa walijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya
Mbeya huku wengine wakipatiwa huduma ya kwanza kisha kuendelea na safari baada
ya kubadilishiwa gari.
Gari hilo lenye namba za
usajili T 887 AYG liliharibika vibaya na kushindwa kuendelea na safari ndipo
lilipoletwa basi lingine kampuni hiyo hiyo ya Sabena kwa ajili ya kuendelea na
Safari.
Kondakta wa Basi hilo Seif
Salum(34) amesema chanzo cha ajali hiyo ni ubovu wa gari uliosababisha kupasuka
kwa mpira wa Breki hivyo gari kushindwa kusimama na kutumbukia mtaroni.
Amemtaja Dereva wa basi hilo
kuwa ni Suddy Hussein ambaye inasadikika kuwa alikimbia baada ya ajali hiyo ingawa
kondakta alitoa taarifa kuwa kafuata matibabu Hospitalini.
Picha na Mbeya yetu.
No comments:
Post a Comment