Msanii wa bongo fleva mwenye mafanikio makubwa zaidi Tanzania Diamond Platnumz, jana (June 19) amekutana na aliyekuwa rafiki wa karibu wa marehemu Albert Mangwea anayefahamika kama M 2 The P, na inavyoonekana wana mpango wa kufanya kitu pamoja.
Platnumz ameweka picha katika website yake akiwa na M 2 The P ambaye sasa anaonekana mwenye furaha inayoashiria kuimarika zaidi kwa afya yake.
Katika picha hizo Diamond aliandika,
“Siku ya jana katika mishe mishe zangu nilikutana
na ndugu yetu na mwanmuziki mwenzetu,M 2 the P ambae
alikuwa ni mtu wa kalibu na
marehemu Ngwair…kukutana kwetu tulipata fursa ya
kuzungumza mengi nna Mungu akipenda..maybe we gonn do
something”
Diamond-3
Hit maker huyo wa ‘Kesho’ yuko katika maandalizi ya mwisho ya safari yake ya Comoro anayotegemea kwenda kufanya show hivi karibuni.
Magazetini Leo Januari 17, 2025; Mauaji ya Kutisha
-
Copyright 2007-2021 @KAJUNASON BLOG
6 hours ago


No comments:
Post a Comment