Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, June 11, 2013

IGP MWEMA AKUTANA NA MAASKOFU KATOLIKI JIMBO KUU DAR


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema akiwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini Kardinali Pengo wakiingia katika ukumbi wa mkutano wakati wa kikao cha Mashauriano kati ya Jeshi la Polisi na viongozi wa makanisa ya kikatoliki uliofanyika jijini Dar es Salaam.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Dar es Salaam Mwadhama Kardinal Pengo amesema viongozi wa dini hawawezi kukwepa jukumu lao la kuhakikisha kuwa uhalifu unapungua hapa nchini kwa kuwa jukumu hilo linaanzia kwao.
Pengo alisema kuongezeka kwa uhalifu ni changamoto kwa viongozi wa dini kwa kuwa wao ndio wenye kazi ya kujenga maadili katika jamii na polisi kusimamia sheria na kuwachukulia hatua wale wanaokaidi
Hayo yalisemwa wakati wa kikao cha mashauriano kati ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema vongozi wa dhehebu la Romani Katoliki uliofanyika jijini Dar es Salaam .
Naye Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Dar Es Salaam, Mhashimu Eusebius Nzigilwa akisoma maazimio yaliyofikiwa katika kikao hicho alisema wamekubaliana kuziimarisha kamati za ulinzi na usalama katika nyumba za ibada zilizopo hivi sasa wakati wakiendelea kupata mafunzo ya ukamataji salama kutoka Jeshi la Polisi.
“Parokia ambazo hazijaunda kamati za ulinzi na usalama zihakikishe zinafanya hivyo ndani ya mwezi huu na zile ambazo zimeundwa lakini hazifanyi kazi mziimarishe ili kwa pamoja tuwe salama katika nyumba zetu za ibada”Alisema Askofu Nzigilwa.

Katika mazungumzo hayo IGP Said Mwqema alisema kwamba Viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika jamii ya kupunguza uhalifu kwa kuwa wao wanauwezo wa kuwabadili watu kimatendo na kifikra  kwa kufanya doria ya mwili na roho kwa pamoja hivyo wanaweza kusaidiana na Polisi katika kupunguza
uhalifu.

No comments:

Post a Comment