Hatimaye Askofu Zachary Kakobe
amejitokeza katika ibada ya Jumapili hii na kuzungumza mengi kuhusiana na wito
wake wa kuhubiri na kufundisha utakatifu Duniani, Askofu Kakobe alianz aibada
hiyo ya mahubiri kwa kusema, mtu ukiwa na pesa unaweza kupata chochote cha hapa
Duniani, lakini huwezi kupata vitu vya rohoni kwa njia ya pesa, vitu vya rohoni
unaweza kuvipata kwa njia ya maombi pekee yake, aliyasema hayo Kakobe kwa
kusoma maandiko ya kitabu cha Mathayo 6:33
Mungu wakati anampa ramani na
agizo la kwenda kwangu kuhubiri Canada, tangu nipewa agizo hilo hadi leo,
imekwisha pita miaka mitatu, wakati wote huo nipo kimya nautafuta uso wa Mungu
nikimwomba anipe karama na vyote vinavyohitajika kwaajili ya wale walioko huko ,
wakati napewa maelekezo hayo nikama vile mtume Petro alivyokuwa anapewa maagizo
ya kwenda kuvua samaki
Ibada hiyo iliambatana na shangwe
na vigelegele vingi vya; haleluya haleluya amen amen na wengine kutokana na furaha
iliyokuwepo, walipiga vigelegele vya Yesu Yesu Yesu
Kuna watu wanaeneza uongo eti
kakobe katoroka, ndugu zangu nitoroke kwenda wapi, mimi sijatoroka, lakini
nakwenda Canada kwaajili ya kulitimiliza agizo la Mungu alilonipa, nimekwisha
imaliza kazi hapa Tanzania, nimekwisha kuhubiri vijiji karibia vyote hapa
Tanzania, na nimehubiri kwa njia ya Tv kwa miaka mitano kwa gharama kubwa,
fedha zilizotumika kulipia vipindi vya Tv kwa muda wote huo, ni zaidi ya
shilingi bilioni tatu, nimekwenda Kenya, Zambia, Congo, Burundi nk kwahiyo
nimefanya kazi na kwa hapa kwenda nikama kazi nimeimaliza, na sasa napaa kwenda
Canada ambako ndio miisho ya Dunia
Wanangu Mungu ametuinua sana, ule
uwanja nitakao utumia kule Canada ni uwanja wa kisasa sana ambao umezinduliwa
miaka ya hivi karibuni, na sio uwanja unaoweza kutumiwa na mhubiri yeyote,
lakini kwakuwa ni mpango wa Mungu, sisi Fgbf tunakwenda kuutumia na wazungu
wataokoka kwa wingi wao. Katika mkutano huo Kakobe atakuwa akihibiri pamoja na
wahubiri mbalimbali kutoka Marekani nan chi nyinginezo, pia mwimbaji mashuhuri
Duniani Don Moen naye atakuwepo
Canada ni nchi tajiri sana na
watu wenye kujivunia utajiri wao, na ndio maana, hata Rais wetu akienda kule
huwa hapokelewi na mkuu wanchi ile, wanaompokea ni watu wa kawaida kama vile viongozi
wa kitongoji furani, pamoja na yote waliyonayo, kakobe anakwenda kuwahubiri
Injili na kuwangoza sala ya toba. Na kwa taarifa yenu nimekataa kuhubiri kwa
kiingereza, safari hii nahubiri kwa Kiswahili kwa lengo la kujenga utamaduni wa
kitanzania na kuiletea heshima Tanzania
Kwahiyo mkisikia mtu anasema Kakobe
ametoroka, huyo mnapaswa kumpuuza kabisa kwasababu huyo anakuwa ni shetani,
hata mimi ningekuwa shetani lazima ningezungumza maneno kama hayo, kwavile
shetani anajua kinachokwenda kufanya kule
Wakati hayo yakienda kutendeka
kule Canada, sauti ya kanisa imepata taarifa kwamba, Askofu Kakobe wiki mbili
zilizopita alipatwa na msiba wa kuondokewa na mama yake mzazi, kifo na msiba
huo, ulitokea huko Mkoani Kigoma, katika kijiji cha Kakonko, ambako ndio kwao
na Kakobe, kwa taarifa ni kwamba Askofu Kakobe hakwenda kuaga wala kumzika mama
yake mzazi, kutokana na majukumu aliyonayo kihuduma na maombi mazito kwaajili
ya kuhubiri Injili Canada na Duniani kote.
Kwahakika Kakobe ni mtumishi
aliyejitoa kipekee sana kutenda kile alichokiamini, sio raisi kwa mtu mwingine
kuwa na viwango vya juu kiasi hiki ikiwa haujajitoa kama Kakobe, tunaamini
kwamba atakuwa kielelezo kwa wengi na hasa kanisa lake na wachungaji wa kanisa
lake, ya kwamba kama kuna jambo la kiroho basi ni muhimu walitangulize hilo
kuliko kwenda kuzika wazazi wao!
Sauti ya kanisa, inamtakia safari
njema Askofu Kakobe na kumtakia kila la heri huko Canada, kama alivyosema mwenyewe
kwamba, anakwenda kuchukua medali ya dhahabu, basi sauti ya kanisa inamtakia
heri, sio dhahabu moja bali ziwe nyingi
No comments:
Post a Comment