NA THE HABARI
WANASEMA
maji ni uhai, kinyume chake bila maji hakuna uhai wa mwanadamu na hata
wanyama. Kimsingi kauli hii inaonesha umuhimu wa maji katika maisha ya
kila siku ya binadamu na hata viumbe wengine. Shughuli nyingi
zinazofanywa na mwanadamu kila siku zinategemea uwepo wa maji. Matumizi
ya maji kwa shughuli za binadamu hayaepukiki. Na hata katika mwili wa
binadau ni muhimu zaidi, kama huto yaitaji maji kwa kunywa utayahitaji
kwa kuoga na usafi wa shughuli nyingine.
Kwa mantiki hiyo hali yoyote ya upatikanaji ngumu ya upatikanaji wa maji unaathiri maisha ya kila siku ya mwanadamu. Shida ya huduma ya maji eneo fulani huweza kuchangia ugumu wa maisha kiasi fulani. Shida ya maji maeneo mengine huweza kupunguza shughuli za uzalishaji mali, hii ni kutokana na muda mwingi kupotezwa na jamii kwa ufuatiliaji wa maji hasa maeneo ya vijijini.
Hali kama hii ya shida ya huduma ya maji ndiyo inayowakumba wananchi wa vijiji anuai vya Kata ya Kishapu, Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga. Kata ya Kishapu ina vijiji nane yaani Mhunze, Lubaga, Isoso, Mwanuru, Migunga, Mwamagembe, Mtaga, na Kishapu yenyewe.
Japokuwa vijiji vingi vina shida kubwa ya huduma za maji, lakini hali ya ugumu wa upatikanaji huduma hizo hutofautiana kutoka kijiji kimoja hadi kingine. Kati ya vijiji vyote nane vijiji vinne ndio vyenye shida ya maji zaidi. Vijiji hivyo ni pamoja na Lubaga, Isoso, Mwanuru na Kishapu yenyewe.SOURCE LUKAZA BLOG
No comments:
Post a Comment