Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, June 9, 2013

TBL yakipongeza Chuo cha CBE kwa ubingwa wa Safari Pool


 Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akizungumza na wanafunzi wa wa CBE pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kuwapongeza Chuo cha Biashara cha CBE kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Pool yaliyojulikana kwa Safari Lager Higher Learning Pool Competition 2013 yaliyomalizika juni 2,mwaka huu katika Viwanja vya Leaders jiji ni Dar es Salaam iliyofanyika katika Hoteli ya Chichi Kinondoni .Kulia ni Katibu wa Chama cha Pool Tanzania(TAPA), Amos Kafwinga.
 Wanafunzi wa Chuo cha CBE wakicheza muziki wakati wa hafla ya kuwapongeza Chuo cha Biashara cha CBE kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Pool yaliyojulikana kwa Safari Lager Higher Learning Pool Competition 2013 yaliyomalizika juni 2,mwaka huu katika Viwanja vya Leaders jiji ni Dar es Salaam iliyofanyika katika Hoteli ya Chichi Kinondoni .
 Wanafunzi wa Chuo cha CBE wakipata kinywaji wakati wa hafla ya kuwapongeza Chuo cha Biashara cha CBE kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Pool yaliyojulikana kwa Safari Lager Higher Learning Pool Competition 2013 yaliyomalizika juni 2,mwaka huu katika Viwanja vya Leaders jiji ni Dar es Salaam iliyofanyika katika Hoteli ya Chichi Kinondoni .
Wanafunzi wa Chuo cha CBE wakichukua chakula kinywaji wakati wa hafla ya kuwapongeza Chuo cha Biashara cha CBE kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Pool yaliyojulikana kwa Safari Lager Higher Learning Pool Competition 2013 yaliyomalizika juni 2,mwaka huu katika Viwanja vya Leaders jiji ni Dar es Salaam iliyofanyika katika Hoteli ya Chichi Kinondoni .

Na Mwandishi Wetu.
 
KAMPUNI ya Bia Tanzaina (TBL) kupitia Bia yake ya Safari Lager imewapongeza mabingwa wa Taifa wa mashindano ya Pool,Chuo cha Biashara cha Dar es Salaam(CBE) yaliyojulikana kwa “Safari Lager Higher Learning Pool Competition 2013 yaliyomalizikika mwanzoni wa mwezi juni katika Viwanja vya Leader jijini Dar es Salaam 
 
Akizungumza na wachezaji wa timu ya CBE pamoja na wanafunzi wenzao waliokuwa wamealikwa kwenye hafla ilifanyika katika Hoteli ya Chichi Kinondoni jijini Dar es Salaamo,Meneja wa Bia ya Saafari Lager, Oscar Shelukindo alisema ni furaha ya pekee kuona mchezo wa pool unakua mara baada ya kuupeleka katika wanafunzi wa elimu ya juu na kuonekana unahamasa kubwa hata kupelekea kuyashinda mashindano ya kitaifa.
 
Alisema Shelukindo,Safari lager itahendelea kudhamin I mchezo huo mpaka jamii itambue kuwa ni mchezo kama michezo mingine na si mchezo wa kihuni kama taswira ilivyokuwa inaonyesha hapo awali.
 
Shelukindo alisema ni jukumu lenu sasa kuhakikisha mnakuwa mabalozi wazuri wa kuusapoti mchezo huu na kuwafundisha wengine na la zaidi kuendelea kunywa Bia ya Safari Lager Bia namba moja Afrika ili iendelee kudhamini mashindano hayo.
 
Shelukindo aliwapongeza CBE kwa kutwaa ubingwa na kuwatia hamasa wajipange mapema mwaka ,kesho ili ubingwa huo uendelee kubaki CBE na Mkoa wa Dar es Salaam uendelee kupata sifa nzuri ambako ndiko makao makuu ya uzalishaji wa Bia ya Safari Lager.
 
Nae Naahodha wa timu ya CBE,Abubakari Amri aliwashukuru  na kuwapongeza Chama cha mchezo wa Pool Tanzania (TAPA) kwa kuendeleza mchezo wa Pool Tanzania lakini zaidi aliwapongeza Bia ya Safari Lager kwa kudhamini mchezo wa Pool na kufafanyia tafrija ya pongezi ambayo hawakuitegemea na kuwaomba waendelee kudhamini na wao kama CBE waliahidi kuendelea kushikilia ubingwa huo si mwaka kesho tu bali na miaka yote inayokuja. 
 
Chuo cha Biashara cha CBE kwa kutwaa ubingwa Juni 2 mwaka huu kilizawadiwa fedha taslimu shilingi 2,500,000.pamoja na Kikombe na mshindi wa pili katika mashindano hayo alikuwa ni Mzumbe Mbeya na Mzumbe Morogoro ilikamata nafasi ya tatu ambapo mabingwa watetezi SAUT Mwanza walitupiliwa mbali na kushika nafasi ya nne.

No comments:

Post a Comment