KWA MSAADA WA SPORTSMAIL.COM
MSHAMBULIAJI
Lionel Messi amepiku rekodi ya Diego Maradona ya kufunga mabao katika
timu ya taifa ya Argentina, baada ya jana usiku kufunga mabao matatu
peke yake akiiwezesha nchi yake kuibwaga Guatemala 4-0 katika mchezo wa
kirafiki.
Nyota
huyo wa Barcelona sasa analingana kwa mabao na Hernan Crespo, 35 kila
mmoja lakini anazidiwa kwa mabao 21 na gwiji Gabriel Batistuta.
Watu
wamekuwa wakibishana sana juu ya uwezo wa Messi na Maradona kwamba nani
zaidi kati yao, lakini nyota wa Barca akiwa na umri wa miaka 25 tu
anaonyesha anaweza kustaafu akiwa mfungaji bora wa kihistoria kwa nchi
yake.
kazi nzuri: Lionel Messi akishangilia na Sergio Aguero (kushoto) na chini akiifungia timu yake kwa Penalti
Amepitwa:
Diego Maradona ameifungia mabao 34 Argentina na alikuwa anashika nafasi
ya tatu katika orodha ya wafungaji wa kihistoria
Utamchagua nani? Ubishani kwamba nani zaidi kati ya Messi (kulia) na Maradona (kushoto)
Alirejea kwenye kikosi cha kwanza baada ya kuwekwa benchi katika mechi mbili zilizopita kutokana na kuwa majeruhi.
Alifunga
bao la kwanza kwa shuti la mbali, kabla ya kumtengenezea nafasi ya
kufunga bao la pili Augusto Fernandez kisha akafunga kwa penalti
kufikisha idadi ya mabao ya Maradona kabla ya mapema kipindi cha pili
kufunga bao la kumpiku gwiji huyo, akiunganisha pasi ya Ezequiel Lavezzi.
Batigol:
Gabriel Batistuta ndiye mfungaji bora wa kihistoria wa Argentina akiwa
mbele ya Hernan Crespo (chini) na sasa na Messi pia
Lakini
kocha wa zamani wa ufiti wa Argentina, Fernando Signorini ameonya
kwamba Messi anaweza akawa hayuko vizuri wakati wa Fainali za Kombe la
Dunia mwakani kutokana na kutumika sana.
“Kabla,
Miaka ya 60 na 70, wachezaji walikuwa wanacheza mechi 80 hadi 90 kwa
mwaka, lakini (Messi), ni nambari moja duniani, anacheza mechi zaidi ya
120 kama ukihesabu mechi zake za Barcelona na timu ya taifa,”alisema na
kunukuliwa na Marca.
“Messi
amecheza miaka mitatu bila kuumia, lakini miezi miwili na nusu
iliyopita aliumia misuli kabla ya Nusu Fainali ya Kwanza ya Ligi ya
Mabingwa dhidi ya Bayern Munich nchini Ujerumani, na akawekwa benchi
katika mchezo wa marudiano. Kisha akaumia tena,”alisema.
Wasiwasi: Messi anaweza asiwe vizuri kwa asilimia 100 wakati wa Kombe la Dunia kwa sababu ya kutumika sana
No comments:
Post a Comment