Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, June 26, 2013

MAANDALIZI YA SOKA LA UFUKWENI YAZIDI KUPAMBA MOTO - VIWANJA VYAANZA KUTENGENEZWA

Maandalizi ya mradi wa Tanzania Beach Soccer unaoratibiwa na kampuni ya Prime Promotion kwa kushirikiana na shirikisho la soka nchini TFF yanaendelea vizuri sana.
Kwa mujibu wa mwakilishi wa Primetime Promotion Shaffih Dauda ni kwamba sasa mradi huo umefikia katika hatua nzuri ya ujenzi wa viwanja vitakavyotumika katika michuano ya mchezo huo.
"Kwa sasa tumeanza kazi ya kutengeneza viwanja pembezoni mwa ufukwe wa bahari hindi katika eneo la Mikocheni ulipo mgahawa wa Escape 1. Tunashukuru ushirikiano mzuri tunaopata kutoka kwa TFF chini ya mkurugenzi wa ufundi Sunday Kayuni. Kama maandalizi na mipango yote ikienda kama ilivyopangwa tunategemea michuano hii itaanza mwishoni mwa mwaka huu."


Utengenezaji wa viwanja ukiendelea Mikocheni pembezoni mwa bahari ya Hindi.source shaffih dauda

No comments:

Post a Comment