Mkuu
wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akikagua Gwaride la Mapokezi mara
alipowasili katika Makao makuu ya Jeshi la Oman kuanza Ziara ya kikazi
nchini Oman, kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Oman Luteni Jeneral Ahmed bin
Harith Al Nabhani.
Mkuu wa Majeshi akiwa katika mazungumzo na Mwenyeji wake.
Mku wa Majeshi
Jenerali Davis Mwamunyange
katikati)akiwa katika mazungumzo na Waziri katika Ofisi ya Mfalme Mhe.
Sultan bin Mohamed Al Nuamani (kulia), akishuhudia ni Balozi wa Tanzania nchini
Oman Mheshimiwa Balozi Ali Ahmed Saleh (kushoto)
Mkuu wa
Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange
akipokea taarifa kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Oman Mhe. Balozi
Ali Ahmed Saleh alipotembelea ofisi za
ubalozi wa Tanzania nchini Oman.
Mheshimiwa Balozi Ali
Ahmed Saleh akimuonyesha Mkuu wa Majeshi mchoro wa litakalokuwa jengo la
Ubalozi wa Tanzania nchini Oman.
Mheshimiwa Balozi Ali
Ahmed Saleh mstari wa mbele kulia akiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa
majeshi na ujumbe wake.
Mkuu wa
Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange
katika picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo cha Uongozi na kamandi cha Oman.
Mkuu wa Majeshi
Jenerali Davis Mwamunyange akisalimiana
na Meja Saif Wibonela, Mwanafunzi wa kitanzania anaesoma hapo.
Mkuu wa Majeshi
Jenerali Davis Mwamunyange (watano
kutoka kushoto waliokaa ) katika picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo
cha Anga cha Oman (watatu kutoka kushoto
waliokaa) ni Balozi wa Tanzania nchini Oman Mhe. Balozi Ali Ahmed Saleh.
Mkuu
wa majeshi ya Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange, alifanya ziara ya
Kikazi nchini Oman kuanzia tarehe 23 hadi 27 Juni 2013 kwa Mwaliko wa
mwenyeji wake Luteni Jenerali Ahmed bin Harith Al Nabhani.
Ziara
hii ilikuwa na madhumuni makuu ya kuimarisha uhusiano wa kindungu
uliopo baina ya Oman na Tanzania kupitia sekta ya ulinzi na kuanzisha
uhusiano wa karibu na ushirikiano baina ya vyombo hivi vya ulinzi kati
ya Tanzania na Oman.
Katika
ziara hii Mhe. Jenerali Mwamunyange alikutana na kufanya mazungumzo na
Mwenyeji wake Luteni Jenerali Ahmed bin Harith Al Nabhani na pia
kukutana na Waziri katika Ofisi ya Mfalme Mheshimiwa Luteni Jenerali
Sultan bin Mohamed Al Nuamani .
Mbali
na kukutana na viongozi hawa wa Oman, Mkuu wa majeshi alipata nafasi
kutembelea maeneo kadhaa kujonea shughuli mbalimbali za Jeshi la Oman,
alitembelea makumbusho ya Jeshi la Oman, Chuo cha Uongozi na kamandi
cha Oman, Chuo cha Jeshi la Anga, Hospital ya Jeshi , Makao makuu ya
Jeshi la Askari wa Miguu pamoja Makao makuu ya Jeshi la Majini.
Katika
maeneo yote aliyotembelea Mheshimiwa Mkuu wa Majeshi alifurahishwa sana
na shughuli za jeshi la Oman na kuridhika na hatua iliyopigwa na Jeshi
la Oman. Mkuu wa majeshi pia alitembelea ofisi za Ubalozi wa Tanzania
nchini Oman kujionea shughuli mbalimbali za Ubalozi na pia kuhudhuria
hafla ya chakula cha Usiku kilichoandaliwa kwa heshima yake nyumbani kwa
Mheshimiwa Balozi.
credit: Michuzi matukio blog
No comments:
Post a Comment