Watalii
wengi hutembea nusu uchi wakati wanapotembelea fuzo za bahari,Serikali ya Qatar
imezindua kampeini ya kuwasihi watalii kuvalia mavazi ya heshima wanapokuwa
katika maeneo ya umma na pia kuheshimu maadili ya kiisilamu nchini humo.
Kupitia
kwa Twitter na Instagram, serikali hiyo inaweka picha zinzoonyesha ambavyo
watalii wanapaswa kuvalia wakiwa nchini humo pamoja na kuonyesha mavazi
yasiyoruhisiwa.
Hii
ni kampeini ya kupitia kwenye mitandao ya kijamii kwa watu wanaonuia kusafiri
kwenda Qatar.Mavazi kama nguo fupi, zisizo na mikono mirefu na vitopu vifupi,
yameharamishwa, wakati wanaume hawaruhusiwi kuvalia kaptula na vesti huku
wakionyesha vifua vyao.
Kauli
mbiu ya kempeini hiyo ni'' Ukiwa Qatar wewe ni mmoja wetu. Tusaidie kuendeleza
maadili na utamaduni wa Qatar , tafadhali valia mavazi ya heshima. ''Kampeini
hiyo inawaomba watu kufunika mabega yao na magoti na kujizuia kuvalia
stockings.Kituo cha utamaduni wa Qatar, kimewahi kuzindua kampeini kama hii ili
kuwafunza watalii kuhusu mavazi yao.
Picha Ya Chini Ndio zinazotumiwa na Qatar
kuhamasisha watalii dhidi ya kuvalia nguo zisizo na heshima
"kiwango cha watu kuvalia
nguo zisizo za heshima, kimeongezeka hasa katika maeneo ya umma ikiwemo katika
maduka makubwa ya kifahari,'' alisema Nasser Al Maliki, afisaa mkuu wa
mawasiliano katika kituo hicho."hatutaki watoto wetu kuishi katika
mazingira kama haya na kuweza kujifunza mambo yasiyokubalika na ndio maana
tunafanya kampeini hii. ''
Qatar, ni mwenyeji wa michuano ya
kombe la dunia mwaka 2022 na ina takriban watu milioni 2 na pia hutumia sheria
ya kiisilamu katika mfumo wake wa sheria.Raia wa Uingereza 17,500, wanaishi
katika nchi hiyo na nchi hiyo pia hupokea wageni 40,000 kila mwaka.Kuvalia nguo
zinazoonekana kukosa heshima ni kinyume na sheria sawa na ilivyo kutoa matamshi
ya matusi au kufanya kitendo chochote kisichokubalika katika sehemu ya umma.Ikiwa
atapatikana na hatia mtu anaweza kufungwa jela miezi sita au kutozwa faini.
No comments:
Post a Comment