Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, June 11, 2013

MWENYEKITI WA CCM JAKAYA KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM KUPOKEA RASIMU YA KATIBA MPYA


 Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akiongoza kikao cha Maalum ya CCM ‘Kamati Kuu’ kilichokutana jana usiku mjini Dodoma kwa ajili ya kuipokea Rasimu ya Katiba mpya, iliyosomwa hivi karibuni.
 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imekutana jana tarehe 10/06/2013 chini ya
uenyekiti wa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Kikao hicho
kilikuwa cha siku moja na maalum kwa ajili ya kupokea rasimu ya katiba mpya.
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imekutana jana tareh 10/06/2013 chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Kikao hicho kilikuwa cha siku moja na maalum kwa ajili ya kupokea rasimu ya katiba mpya.
Kamati Kuu inaipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini kwa kazi nzuri na kukamilisha kazi kwa wakati.
Kamati Kuu imepokea rasimu hiyo na kuelekeza kuwa; Kwa kuwa rasimu hii ni ya kwanza ambayominapelekwa kujadiliwa tena kwa wananchi kupitia mabaraza mbalimbali ya katibam baada ya kuisha kwa hatua ya kutoa maoni.
Kamati Kuu imekiagiza Chama kijipange kuijadili rasimu hiyo ndani ya Chama kama baraza la kitaasisi la katiba na kuwataka wanachama na wapenzi wa CCM wajitokeze kwa wingi na kushiriki kwenyemabaraza haya Ushiriki huu wa CCM baada ya kupokea rasimu umekusudia kushirikisha wanachama wetu kwenye ngazi ya tawi, wilaya, mkoa na Taifa.

Lakini pia Jumuiya za CCM zimekusudia kushiriki kama mabaraza ya Katiba na hivyo kuongeza ushiriki wa wanachama na wapenzi wa CCM katika mchakato huu.
CCM kama baraza la katiba la kitaasisi litaipitia rasimu iliyowasilishwa kifungu kwa kifungu na kwa kuzingatia maoni ya CCM yaliyotolewa mwanzoni kabisa mwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba, wanachama wetu watashiriki kutoa maoni yao.
Pamoja na kazi nzuri ya Tume ya Mabadiliko ya katiba, Kamati Kuu inaiomba Tume hiyo kueleza vizuri mchakato mzima kutoka rasimu ya kwanza mpaka rasimu ya mwisho ili kuondoa mkanganyiko kwa wananchi juu ya mchakato mzima hasa baada ya rasimu ya kwanza kutoka.
Kamati Kuu inawasihi Watanzania kushiriki tena kwenye kutoa maoni kupitia mabaraza ya katiba kwa rasimu ya kwanza, bunge maalum la katiba kwa rasimu ya pili na kupitia kura ya maoni kwa rasimu ya tatu, kwa amani,utulivu na kuvumiliana ili mwisho wa siku tupate Katiba nzuri ya nchi yetu kwa masilahi ya Watanzania walio wengi.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Moses Nnauye, akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo mchana kuhusu kikao hicho cha Kamati Kuu ya CCM, kilichokutana jana usiku.
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu, waliohudhuria kikao hicho jana usiku.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Mwigulu Nchemba, akiperuzi ‘mambo flani’ katika simu yake ya mkononi, wakati akiwa ukumbini humo kwenye Kikao cha Kamati Kuu kilichokutana jana usiku.
 Sehemu ya Wajumbe wa Kikao hicho ambao wengi wao ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment