Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, June 8, 2013

MWIGULU NCHEMBA AONGOZA KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA KALOLENI ARUSHA



Naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania bara akiwasili viwanja vya kata ya kaloleni-stendi jioni ya leo kwa ajili ya mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Udiwani kata ya kaloleni Jijini Arusha


Naibu katibu Mkuu wa CCM Mh.Mwigulu Nchemba akilakiwa na Bibi mwanachama wa CCM eneo la mkutano kaloleni jijini Arusha

Naibu katibu mkuu wa CCM Mh.mwigulu Nchemba akilakiwa na mgombea UDiwani wa kata ya kaloleni kwa tiketi ya CCM Ndugu Emmanuel Thomas

Naibu katibu mkuu wa CCM Mh.Mwigulu Nchemba akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara kwaajili ya kampeni za uchaguzi wa Udiwani kata ya kaloleni jijini Arusha

CCM inalea na kukuza watoto kwaajili ya taifa lenye Heshima na ustaarabu siku za Usoni.Hawa na Vijana wa CCM wakisoma ngonjera mbele ya naibu katibu mkuu wa CCM Mh.Mwigulu Nchemba

Kushoto ni aliyekuwa diwani wa CHADEMA Ndugu Rehema sasa ni kada mtiifu wa CCM.Kulia ni Mgombea Udiwani kwa tiketi ya CCM ndugu Emmanuel Thomas

Aliyekuwa diwani wa CHADEMA Ndugu Rehema akisalimia wananchi na kuwaomba waachane na CHADEMA ili wapate maendeleo kuanzia ngazi ya kata hadi wilaya na Kitaifa.Amesisitiza CHADEMA ni chama cha watu wachache na chenye mlengo wa maslahi binafsi.Amewaomba wanaarusha kuchana na adha ya kuamrishwa kila kitu na Mbunge wao wa maandamano Ndugu Godbless Lema.Amesema yeye ameshakaa chadema na anajua uchafu wote unaofanyika kuanzia kwa Mwenyekiti wa chama,katibu mkuu wa chama na hata ngazi za chini.Hivyo amewaomba wanaarusha kumchagua diwani wa CCM kwa maendeleo ya kata ya kaloleni

Kada wa CCM Bi.Juliana Shonza akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi kata ya Kaloleni.Bi.Juliana shonza amewaomba wakaloleni na Wanaarusha kuacha kutumika,Kuacha kuwa wafusai wa mtu,Kuacha kuliangamiza jiji la arusha kiuchumi kwa kuendelea kuikumbatia CHADEMA.Amesisitiza yeye alikuwa chadema na alikuwa kiongozi wa juu ndani ya chama ameona namna chama kinavyoendeshwa kwa maslahi ya watu wachache.Hivyo chaguo sahihi kwa wanakaloleni na wanaarusha ni kuipa nafasi CCM kwenye uchaguzi huu wa Udiwani

Bi.Juliana shonza akisisitiza kwamba hakuna chama kama CCM,CCM ni chama chenye mlengo wa kitaifa kimaendeleo.CCM ni chama tawala na kinamaslahi jamii

Huyu kijana alikuwa kamanda wa CHADEMA,amesema aliachana na CHADEMA baad aya kugundua kuwa anapoteza muda wake kuhangaikia watu binafsi na sio maslahi jamii.hapa alikuwa anaonesha barua na hati mbalimbali anazofanyia utapeli Mbunge wa Arusha mjini Ndugu GodBless Lema.Ameeleza namna Lema alivyoweka ARUSHA DEVELOPMENT FOUNDATION mali ya familia yake,Mke wa Godbless lema ndiye Mkurugenzi wa mfuko huo.Hivyo amewasihi vijana wenzake kuachana na CHADEMA,Wafanye chaguo sahihi kwa kumpa kura mgombea wa CCM

Mh.Munge Devotha Likokola akihutubia mamia ya wananchi wa kaloleni waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni za Uchaguzi jijini Arusha kata ya kaloleni.Amesema wanakaloleni wasipoteze muda wao kwa kukipa nafasi chama chochote cha upinzani.Amesisitiza atasaidiana na akiana mama wa kata ya kaloleni keendeleza mifuko ya VICOBA ambayo ipo chini ya serikali ya CCM

Mh.Mbunge Devotha Likokola akimnadi mgombea wa udiwani kata ya kaloleni Ndugu Emmanuel Thomas kwa tiketi ya CCM.Amesisitiza hakuna mtanzania asiyependa kufika ama kuishi Arusha,Lakini kwa huu upuuzi wa CHADEMA wa kuvuruga jijini ni ishara tosha kwamba hawafai hatakupewa nchi.Hivyo wanakaloleni wampe kura diwani wa CCM.


Mh.Mwigulu Nchemba,Naibu katibu Mkuu wa CCM  amehutubia mamia ya wananchi wakata ya kaloleni jijini Arusha jioni ya leo tar.8/6/2013 kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani.Mh.Mwigulu Nchemba ameanza kw akusema uchaguzi unaofanyika sasa kata ya kaloleni ni matunda ya chama mufilisi cha chadema kutotambua haki ya wananchi wanaopiga kura.Amesema CHADEMA walifukuza diwani hapa,je kunahaja ya kuwapa diwani tena?AU  walipowafukuza walikuja kuomba ridhaa ya wananchi wa kaloleni?.Huu ubabe kwenye vyama vya siasa ni wakupinga vikali na njia pekee ni kupiga kura za kutosha kwa mgombea wa CCM.

Naibu katibu Mkuu wa CCM akisisitiza jambo kwa wananchi.Amesisitiza sana kuhusu amani wakati wa uchaguzi na wakati wote wa maisha ya kila siku.Amesema ni ajabu kwa Wana kaloleni na wanaarusha kukipigia kura chama kinachoshabikia maauaji,CHADEMA wanashabikia mauaji,Chadema wanatumia misiba kuhadaa wananchi na kutafuta sifa za kijinga.Pia amewaomba wananchi kulaani vikali tabia ya Mbunge wa Arusha mjini kutumia viroba kama fadhila kwa wananchi waliompigia kura.Amesema thamani ya vijana wa Arusha sio viroba,Thamani ya vijana wa arusha ni maendeleo na kudumisha amani.

Hapa Naibu katibu mkuua alikuwa anauliza,Je CHADEMA wamejenga angalau choo cha jumuia hapa kaloleni?Pia akauliza ni kwanini CHADEMA hawafanyi maandamano wilaya ya Hai na karatu?Akahoji zaidi kwa kusema je kunamzazi anafurahia mtoto wake amwagiwe tindikali.

Naibu katibu Mkuu wa CCM Mh.Mwigulu Nchemba akimnadi mgombea udiwani kata ya kaloleni kwa tiketi ya CCM Ndugu Emmanuel Thomas

Hapa naibu katibu Mkuu wa CCM akimpongeza mgombea udiwani kwa tiketi ya CCM kwa kuamua kujitolea kuwasaidia wanakaloleni na Wanaarusha kwa kupitia CCM chama cha watanzania wote

 Mgombea udiwani kata ya kaloleni Ndugu Emmanuel Thomas  akiomba kura kwa wannachi na kuwaahidi kuendelea kutekeleza ilani ya CCM na kuwaletea maendeleo wanakata ya kaloleni na jiji la Arusha

No comments:

Post a Comment