Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, June 19, 2013

Redds miss tanga kunyakuwa milioni moja


17Na Mwandishi Wetu
ZAWADI kwa mshindi wa Redd’s Miss Tanga 2013 anatarajiwa kuondoka na kitita cha sh.laki tano 500,000 huku msanii wa muziki wa kizazi kipya, Tunda Man, akiongoza kwa upande wa Burudani, katika shindano litakalofanyika Jumamosi katika uwanja wa Mkwakwani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa Mkurugenzi wa Kampuni ya DATK Intertainment Asha Kigundula,alisema kuwa maandalizi ya shindano hayo yapo vizuri ambapo zawadi kwa mshindi wa pili atajinyakulia kitita cha shilingi  300,000.
Kigundula alisema katika shindano hilo mshindi wa tatu atazawadiwa kitita cha shilingi  250, 000 wakati mshindi wa nne na tano wakipata sh.200, 000 kila mmoja na warembo wengine watakaosalia watapata kitita cha sh.laki moja moja kila mmoja 100,000 kama kifuta jasho pamoja na zawadi kwa mrembo mwenye nidhamu ili kuweza kuboresha shindano hilo.
Alisema kuwa hata hivyo kutakuwa na zawadi kwa washindi watatu watakaoibuka katika shindano la vipaji (talent), ambapo mshindi wa kwanza atainyakuliwa kitita cha shilingi 100,000 na mshindi wa pili na watatu kila mmoja atajinyakulia shilingi 50,000.
Kwa upande wa Burudani msanii wa kizazi kipya, Tunda Man, ataongoza safu ya burudani, ambapo itakuwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Dr John, Nabisha kutoka kundi la THT, Fady Dady na wasanii chipukizi kutoka mkoani hapa.
Kigundula alisema shindano hilo linatarajiwa kuanza majira ya saa mbili usiku na kushirikisha warembo 12 ambao watachuana ili kuweza kumpata malkia wa mkoa huu ambaye atauwakilisha mkoa katika mashindano hayo ngazi ya kanda.
Warembo hao ni Hawa Ramadhani (18),Hazina Mbaga (19)Like Abdulraman (19), Irene Thomas(20), Tatu Athumani (19), Winfrida Gutram (21)Lulu Mbonela (19) ,Hazina Daniel (19),Lulu Matawalo(22),Judithi Moleli (21),Neema Jonas na Hawa Twaybu(21)
Wakati huo huo Warembo hao wanaowania Taji la Mlimbwende wameiomba Halmashuri ya Jiji la Tanga kuifanyia marekebisho barabara inayokwenda katika mapango ya Amboni ili iweza kuwa nzuri na ipitike kirahisi nyakati zote.
Ombi hilo lilitolewa na warembo hao mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea mapango hayo ambapo walikwenda kujifunza histori yake pamoja na kuingia mapangoni lengo likiwa ni kujifunza utalii wa ndani ili kuweza kuuutangaza kwa wageni na jamii nzima.
Akizungumza mmoja wa warembo hao, Asia Rashid alisema mapango hayo ni mzuri na endapo yatafanyiwa maboresho ikiwemo kufanyiwa ukarabati barabara inayoelekea katika kivutio hicho itarahisisha usafiri na kupitika bila shida nyakati zote.
Asia alisema wao kama washiriki wa shindano la Redd’s Miss Tanga 2013 wamefarijika sana kupata nafasi ya kutembelea mapango hayo na kuwataka wananchi wa mkoa wa Tanga na wageni wanaoingia mkoani hapa kuwa na utaratibu wa kutembelea vivutio hivyo na kujifunza mambo mwengi ya kale.
Kwa upande wake, Hawa Ramadhani aliwashauri watanzani kujenga utamaduni kutembelea vivutio vya utalii hapa nchini ikiwemo kutunza misitu yetu ili nchi yetu ipendeze na kuwavutia wageni wanaoingia hapa nchini kutoka mataifa mbalimbali.
Hawa alisema wao wamejipanga vema kuhakikisha wanafanya vizuri katika fainali ya shindano hilo ambalo litafanyika June 22 mwaka huu kwenye uwanja wa mkwakwani mkoani Tanga na kushirikisha warembo
Redd’s, Miss Tanga, imedhaminiwa na Al Hayat Ivestment Limited,Dodoma Wine,CXC Africa,Executive  Solutions,Busta General Supply, Mkwabi Interprises,Lusindic Investment LTD,
Lavida Pub,Jambo Leo,Staa Spoti,Five Brothers Cloud’s Media Group,  pamoja  na Blog Michuzi Media Group,Bongostaz.com, Saluti5,Kajuna, JaneJohn, na Kidevu na assengaoscar.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment