“PRESS RELEASE” TAREHE 20. 06. 2013.
WILAYA YA MBEYA MJINI
- MAUAJI YA MTU MMOJA KUFUATIA VURUGU YA WANANCHI WA
KIJIJI CHA LUMBILA WILAYA YA MBOZI KUWASHAMBULIA
ASKARI WALIOKUWA WANAFANYA OPERESHENI.
KIJIJI CHA LUMBILA WILAYA YA MBOZI KUWASHAMBULIA
ASKARI WALIOKUWA WANAFANYA OPERESHENI.
MNAMO TAREHE 19.06.2013 MAJIRA YA SAA 13:00HRS HUKO KATIKA
KIJIJI CHA LUMBILA KATA YA RUANDA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. RAJABU S/O
WILSON MWASHITETE, MIAKA 25, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA LUMBILA
ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA ASKARI POLISI WALIOKUWA KATIKA MSAKO DHIDI YA
WAHALIFU/WAPORAJI KATIKA ENEO LA MLIMA SENJELE .CHANZO NI BAADA YA ASKARI
POLISI WAKIWA KATIKA OPERESHENI ENEO HILO KUZINGIRWA NA KUNDI LA WANANCHI ZAIDI
YA 150 WA KIJIJI HICHO WAKIWA NA SILAHA ZA JADI MAPANGA, MARUNGU, SHOKA NA MAWE
WAKIWAZUIA ASKARI HAO KUKAMATA WAHALIFU NA KUANZA KUFANYA VURUGU BAADA YA KUWA
WAMEKAMATA MALI INAYODHANIWA KUWA YA WIZI AMBAYO NI MAFUTA AINA YA DIESEL MADUMU ZAIDI YA 100, HATA
HIVYO KUFUATANA NA VURUGU ZILIZOJITOKEZA WALIFANIKIWA KUCHUKUA MADUMU MACHACHE
AMBAYO NI MADUMU MATATU YENYE UJAZO WA LITA 60, MADUMU MAWILI YENYE UJAZO WA
LITA 20 NA MADUMU NANE LITA 30 HIVYO UVAMIZI HUO WA WANANCHI NDIO ULIOWAFANYA
ASKARI POLISI WASHINDWE KUCHUKUA VIELELEZO VYOTE. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. AIDHA KATIKA TUKIO HILI
CHARLES S/O JOSE MWAWALO,MIAKA 27,MNYIHA,MKULIMA MKAZI WA
KIJIJI CHA LUMBILA ALIJERUHIWA KWA KUPATA MICHUBUKO TUMBONI AMBAPO UCHUNGUZI
UNAFANYWA KUBAINI NI KITU GANI KILICHOMJERUHI. PIA WANANCHI WALIFUNGA BARABARA
KUU YA MBEYA/TUNDUMA KWA KUWEKA MAWE NA MAGOGO NA KUSABABISHA MSONGAMANO MKUBWA
WA MAGARI BARABARANI. HALI ILIKUWA SHWARI BAADA YA KAMANDA WA POLISI KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI KUFIKA ENEO LA TUKIO NA KUZUNGUMZA NA
WANANCHI PAMOJA NA VIONGOZI WA ENEO HILO KISHA KUFUNGUA BARABARA . ASKARI
POLISI WANNE WALIJERUHIWA KATIKA TUKIO HILO KATI YAO WATATU WALIPATIWA MATIBABU
NA KURUHUSIWA NA ASKARI MMOJA AMELAZWA
HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU ZAIDI . KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA
YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA BADALA YAKE KUWA NA
UTAMADUNI WA KUTATUA KERO/MALALAMIKO YAO KWA NJIA YA MAZUNGUMZO KWA
KUYAWASILISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA. AIDHA ANAWATAARIFU WALE WOTE WALIOWAHI
KUIBIWA/KUPORWA MALI MBALIMBALI YAKIWEMO MAFUTA WAJITOKEZE POLISI KWA AJILI YA
HATUA ZINAZOSTAHILI.
WILAYA YA CHUNYA - KUPATIKANA NA BHANGI
MNAMO TAREHE 19.06.2013 MAJIRA YA SAA 08:30HRS HUKO KIJIJI
CHA MKWANGU WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA DORIA/MISAKO
WALIMKAMATA SEMI S/O KIJA, MIAKA 40, MSUKUMA, MKULIMA, MKAZI WA MKWANGU
AKIWA NA BHANGI DEBE MOJA YENYE UZITO
WA KGM 12 NDANI YA NYUMBA YAKE .
MTUHUMIWA NI MVUTAJI NA MUUZAJI WA BHANGI.
TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA
KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA
MTUMIAJI.
WILAYA YA KYELA -
KUPATIKANA NA BHANGI
MNAMO TAREHE 19.06.2013 MAJIRA YA SAA 12:30HRS HUKO KIJIJI
CHA NJISI WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA
DORIA/MISAKO WALIMKAMATA REBEKA D/O SIMBEYE, MIAKA 40, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI
WA KIJIJI CHA KATUMBA – SONGWE AKIWA NA
BHANGI KETE 9 SAWA NA UZITO WA
GRAM 45 NDANI YA NYUMBA YAKE. MTUHUMIWA NI MVUTAJI NA MUUZAJI WA BHANGI
TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA
KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA
MTUMIAJI.
WILAYA YA MBOZI -
KUPATIKANA NA SILAHA [GOBOLE] BILA KIBALI.
MNAMO TAREHE 19.06.2013 MAJIRA YA SAA 17:30HRS HUKO KIJIJI
CHA MPITO WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MISAKO WALIMKAMATA YAREDI S/O JIMU @ MGARA, MIAKA
45, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA MPITO
AKIWA ANAMILIKI SILAHA AINA YA GOBOLE
MOJA NDANI YA NYUMBA YAKE BILA KIBALI.
MTUHUMIWA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUMILIKI SILAHA BILA KIBALI KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA.
Signed By,
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment