Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, June 25, 2013

TAZAMA PICHA ZA VIJANA 3 WALIOTOKWA NA MATITI NA BAADAE KUFANYIWA OPERATION KUYAONDOA


VIJANA watatu wa familia moja ya  Felipe Ramirez, wamepata balaa kubwa baada ya kuota matiti yaliyosababisha kuchekwa na vijana wenzao waliokuwa wakiwaona kuwa ni mashoga.
Vijana hao kutoka katika Jamhuri ya Dominica ni  Yeuri (17 ), Gabriel (11) na  Daniu Ramírez  (12),  hata hivyo, kwa sasa wanaishi kwa amani baada ya kufanyiwa upasuaji na kuondolewa matiti hayo.


Baba yao mzazi, Felipe Ramirez alifanya jitihada ya kuomba msaada kupitia televisheni na magazeti ili wanawe wafanyiwe upasuaji kwani walikuwa wakiishi katika mateso kwenye jamii yao.
Baada ya kuomba msaada, Mkurugenzi wa Hospitali ya  Marcelino Velez Santana nchini humo, Dokta  Pedro Antonio Delgado


aliamua kuwalipia gharama za upasuaji ambao ulichukua saa mbili.
 Ramirez, alisema: “Wakati wanaingizwa katika chumba cha upasuaji nilikosa raha kwa kuhofia kama watatoka salama nao waliogopa lakini baada ya kutoka, wote tumefurahi sana.”
SOURCE BONGOCLAN TZ


No comments:

Post a Comment