Mratibu wa SPANEST, Godwell ole Maing'ataki
TEMBO
39,000 wameuawa katika kipindi cha mwaka 2009-2012 katika mapori ya
Selous, Hifadhi ya Taifa Ruaha na Pori la Akiba la Rungwe , Kizigo,
Mapori ya Kigosi –Moyowosa na Rukwa katavi.
Hayo
yalielezwa na Mratiba wa Mradi wa Kuboresha Mtandao wa Maeneo ya Hifadhi
Kusini mwa Tanzania (SPANEST), Godwell Meing’ataki alipokuwa
akiwakilisha mada katika kikao cha wadau wa ulinzi wa mali asili
kilichofanyika kwenye ukumbi wa siasa ni kilimo Manispaa ya Iringa.
Alisema
idadi ya Tembo imepungua kutoka 109,000 mwaka 2009 hadi 70,000 mwaka
2012 hivyo kupata idadi ya Tembo walio uwawa kuwa 39.000
Meing’ataki
alisem utafiti unaonyesha kichocheo cha Ujangili ni biashara ya Meno ya
Tembo inayo fanywa na wanunuzi toka China na Mataifa mengine ya Asia
kwasababu ya urahisi wa kupata menoya Tembo.
Uwepo
mpango wa kudumu kuongeza fedha za kusaidia kuwezesha kazi endelevu ya
kupambana na ujangili, Matumizi ya teknolojia ya mawasiliano
Urekebishaji wa sheria ikiwamo na kuanzisha ushirikiano wan a Mtandao wa wadau.
Kwa kuwa
na mahusiano na nchi Mataifa yenye kuhifadhi Tembo kwa ajili ya
kushirikiana katika jukumu la kudhibiti usafilishaji wanyamapori ikiwa
pamoja na ushawishi wa kisiasa na kidiplomasia ni muhimu kufanyika
kampeni za mawasiliano katikanchi wanunuzi wa meno.
Alisema ili kufanikisha yote hayo yafaa kujenga mifumo ya mawasiliano
kuwezesha
Askari wa doria kuwasiliana kwa urahisi katika mapori na vijijini
piakuwepo na Mifumo ya uchunguzi na kubadilishana taarifa kwa kutumia
teknolojia ya kisasa na kuhuisha mitandao ya kikale kwa Mfano mtoa
habari, Kuwageuza majangili kuwa walinzi wakanufaika kihalali zaidi sawa
na watakavyo tumika kwa uhifadhi wa Maliasili. Chanzo: mjengwablog
No comments:
Post a Comment