Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, June 20, 2013

WAMILIKI WA KAMPUNI KUBWA YA Dolce&Gabbana WAHUKUMIWA KWENDA JELA KILA MMOJA MWAKA MMOJA NA MIEZI NANE

Wanamitindo maarufu kutoka nchini Italia Domenico Dolce na mwenzie Stefano Gabbana watu hawa wawili ndo chanzo cha mafanikio makubwa na brand ya Dolce & Gabbana kama inavyojulikana na watu wengi. Wamiliki hawa wawili juzi walihukumiwa na mahakama moja nchini italia kwenda jela kwa mwaka mmoja na miezi nane kila mmoja pia wakaamuliwa kulipa €500,000 kwa kila mmoja.

Mamultimillionaire haya wawili walishtakiwa ndani ya mahakama hiyo kwa kosa la kufanya udanganyi kwa kuficha mamilioni ya pesa ili kutolipa kiwango sawa cha kodi walichotakiwa walipe. 

Inadaiwa kua vyombo vya usalama nchini italia vimekua vikiwachunguza watu hawa kwa zaidi ya miaka sita, tangu mwaka 2006 mpaka mwaka huu walipofikishwa mahakamani na kukutwa na kosa la kutolipa kodi.

Baada ya hukumu hiyo kutolewa, wanasheria wao waliamua kukata rufaa na kwa sheria za Italia hukumu yao imewekwa pembeni kwanza kusubiri rufaa kusikilizwa.source bongoclantz


No comments:

Post a Comment