Fumanizi hilo lilibuliwa ambapo Judith Lekule na mume wa mwanamke aliyetambuliwa kwa jina moja la Pendo
Kwa
mujibu wa vyanzo, Judith yu mbioni kwenda kortini kwa lengo la
kumfungulia mashitaka Pendo akidai alimdhalilisha kwa kudai alimfumania
akiwa na mumewe.“Kuna
watu wanamshawishi Judith eti asikae kimya, aende mahakamani
akamshitaki Pendo kwamba alimdhalilisha kusema alimfumania na mumewe,”
kilisema chanzo hicho.
Hata
hivyo, vyanzo vimeeleza kwamba, Judith anashindwa kuutumia ushauri huo
kutokana na ukweli kwamba, kesi hiyo inaweza kumgeukia mwenyewe kwa
sababu yeye ndiye aliyefumaniwa.
Sambamba
na madai hayo, inasemekana pia kwamba mtaani anapoishi Judith kumekuwa
kuchungu kwake baada ya baadhi ya watu kutumia habari ya kwenye gazeti
kumkejeli na kumuonya akome kuwadandia waume za watu kwani si tabia
nzuri.
“Hali
hiyo ya kunyooshewa vidole na watu inamnyima raha Judith, anashindwa
kutembea kwa uhuru mitaani,” alisema mnyetishaji wetu.
Nao baadhi ya marafiki wa kike wa Judhith wamehuzunishwa na kitendo cha mwenzao kufumaniwa na kupewa kipigo.
Chanzo
kikaenda mbele zaidi kwa kudai kwamba, ndugu wamemtaka Judith aondoke
anapoishi kufuatia kitendo alichokifanya ikielezwa ameitia aibu familia.
Kwa
upande wake, Pendo ameeleza kwamba mumewe alimuomba msamaha na
amemsamehe, yameisha pia akasema baada ya lile fumanizi, Judith
amemfuata nyumbani kwake mara mbili kwa lengo la kuomba msamaha.
“Nimemsamehe Judith lakini bado ana wasiwasi kwani amekuwa akija kwangu na hofu kwamba nitamshitaki katika vyombo vya sheria.
“Cha
ajabu sasa amegeuka na kutoa vitisho, Judith ni rafiki yangu, anajua
alichokifanya ndiyo maana hata wapambe wake wanamshawishi akanishitaki
lakini moyo wake unakuwa mgumu,” alisema Pendo.
No comments:
Post a Comment