Mume akiongea mkewe Mahakamani
Seleman
Yasin (78), mkazi wa Mtaa wa Mtamba, Msasani jijini Dar es Salaam, juzi
Alhamisi aliduwaa baada ya kupata taarifa za mkewe, Saida Abdalah ‘Mama
Hamisi’ (21), kunaswa kwa tuhuma za ukahaba na kupandishwa kizimbani
kwenye Mahakama ya Jiji.
Imedaiwa
mahakamani hapo kuwa Mama Hamisi alinaswa kwenye msako wa machangudoa
uliofanyika usiku wa kuamkia juzi maeneo ya Buguruni.
Akiwa
kizimbani, Mama Hamisi alisomewa shitaka la kujiuza na mwendesha
mashitaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi mbele ya Hakimu Timoth Lyon.
Baada ya
kusomewa shitaka lake, Mama Hamisi na makahaba wengine 13, walikana
kufanya biashara hiyo kesi ikaahirishwa hadi Julai 31, mwaka huu.NA GPL
Mume na mke wakiongea
Hakimu
Lyon aliwaambia washitakiwa kuwa dhamana iko wazi ndipo akatokea mume wa
Saida ‘Baba Hamisi’ na kujitambulisha kisha kuanza kuhangaikia dhamana
ya mkewe ambaye wakati huo tayari alikuwa nyuma ya nondo.
“Yaani we
Mama Hamisi kila siku unanidanganya unauza ubwabwa, Buguruni kumbe
ubwabwa wenyewe ndio huo! Akafyatua tusi,” Baba Hamisi.
Mume akichambua nguo za mkewe
“Kila siku mimi nalala nyumbani na watoto wewe unarudi alfajiri unanidanganya unauza ubwabwa!
“Mimi
machale yalishawahi kunicheza kipindi fulani sema nilikuwa nakuvizia
lakini leo Mungu kanionesha laivu,” alisema Baba Hamisi.
Licha ya
kupandwa na jazba lakini mtu chake, Baba Hamisi alituliza jazba na
kutaka kumchomoa kipenzi chake kwa dhamana lakini alishindwa kutimiza
masharti.
Makahaba wenzie wakiongea
Kwa kuwa
Baba Hamisi alikuwa na safari ya muhimu ya mkoani ikabidi aondoke na
kumuachia nguo za sikukuu alizonunua kwa ajili ya mtoto wao, Hamisi.
Akizungumza
na paparazi wetu, Baba Hamisi alisema yeye hakuwa akifahamu kama mkewe
anajiuza hivyo tukio hilo lilisababisha apigwe na butwaa.
Mpaka
tunaelekea mitamboni, Mama Hamisi alikuwa akisubiri karandinga la
kumpeleka Gereza la Segerea mpaka kesi hiyo itakapotajwa tena.
No comments:
Post a Comment