Dayna akiweka Mshumaa juu ya Kabuli
Mwimbaji wa nyimbo za mafungu ya nyanya, Fimbo ya mapenzi, Nivute
kwako na ule unaotamba sasa wa Leo, Dayna Nyange mkali wao, ndani ya
mwezi mtukufu, amefanya ziara ya kumkumbumbuka na kutembelea kaburi
alilozikwa mwanamuziki mwenzie toka Morogoro, Albert Mangwea
Dayna ameonekana katika kabuli la Mangwea, mwanzoni mwa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Akizungumza
na mwandishi wa Habari hii mara baada ya tukio, Dayna amesema Albert
Mangwea ni mmoja ya wasanii aliokuwa nao karibu sana na alikuwa
akimsaidia kwa mambo mengi sna katika mziki
"Unajua Albert Mangwea ni zaidi
ya msanii mwenzangu, alikuwa kama ndugu kwangu. Albart alikuwa
akinishauli mambo mengi sana juu ya mzikim na hata maisha pia. Hivyo ni
wajibu kwangu kumkumbuka mara kwa mara. Pia kitu ambacho hukijui, Ngwea
ni mmoja ya wasanii walionisaidia sana hasa kusambaza wimbo wangu huu
wa sasa nilioimba na Mr: Blue - Leo. sitamsahau my Brother Ngwea na
ndiyo maana ndani ya mwezi mtukufu nimetenga siku ya leo kuja
kumtembelea. Pumzika kwa amani japo pengo lako bado lipo'' Amemaliza
huku akibubujikwa na machozi.
Dayna akipiga saluti ishara ya kumkubali Marehemu Albert Mangwea
Pumzika kwa amani Ngwae.
No comments:
Post a Comment