skip to main |
skip to sidebar
MWISHO UNAKARIBIA: MCHUNGAJI WA KANISA LA KILOKOLE MBALONI KWA KUMLAWITI MTOTO
MCHUNGAJI
wa kanisa moja la kilokole lililopo Kichangani, Majohe, Dar aliyetajwa
kwa jina moja la Benard anadaiwa kutiwa mbaroni kwa tuhuma za ulawiti wa
mtoto wa kiume (jina tunalo) mwenye umri wa miaka 15.
Hivi
karibuni, gazeti hili lilipenyezewa kuwepo kwa sakata hilo ambapo
lilitinga eneo la tukio na kuweka ‘patroo’ ili kunasa habari kamili.
Kwa
mujibu wa mdogo wa mchungaji huyo aliyejitambulisha kwa jina la Hamis,
kaka yake huyo alikamatwa wiki iliyopita baada ya watu waliojitambulisha
kuwa ni askari kufika nyumbani na kumuweka chini ya ulinzi.
Alisema
kuwa katika kuishi na kaka yake huyo, aliwahi kumuona huyo mtoto
anayedaiwa kulawitiwa mara moja tu kwani yeye bado ni mgeni.
Kwa
mujibu wa dogo aliyedaiwa kuingiliwa, alikutana na mchungaji huyo mwaka
jana maeneo ya Stendi ya Banana-Ukonga, Dar ambapo alimuomba na
kumwambia kuwa alikuwa anatafuta mtoto wa kumfanyia biashara ya mayai
huko Majohe nyumbani kwake.
Alisema kuwa alikataa na kumwambia hawezi kwenda naye bali aende akazungumze na wazazi wake nyumbani.
Alisimulia
kuwa baada ya hapo, aliongozana na baba mchungaji hadi kwa wazazi wake
ambapo walikubaliana kuwa kila mwezi atamlipa mshahara wa shilingi
30,000.
Baada
ya makubaliano hayo ‘dogo’ alisema kuwa aliondoka na mchungaji na baada
ya kukaa kwa muda mfupi huku akiendelea na biashara ya mayai, mchunga
kondoo huyo wa Mungu alianza tabia ya kumfanyia unyama huo huku
akimdanganya kuwa atampa simu.
“Kuna wakati kweli ananipa simu kwa muda na kuninyang’anya.
“Kwa siku moja alikuwa ananiingilia mara mbili, asubuhi na jioni,” alisema mtoto huyo kwa uchungu.
Alisema kuwa baba mchungaji aliendelea kumfanyia ‘usodoma’ kwa muda mrefu.
Alisema baada ya kufika nyumbani kwa wazazi wake, mama yake alimgundua na kumtaka kueleza ukweli.
“Nilimweleza
baba na mama jinsi mchungaji anavyonifanyia ukatili, walimwita nyumbani
wakiwa tayari wameshaandaa polisi jamii, alipofika aliwekwa chini ya
ulinzi lakini aliwaomba msamaha polisi jamii hao pamoja na wazazi huku
akiahidi kutorudia tena.
“Kila mtu alikubaliana na msamaha na kumpa masharti kwamba afilisiwe vitu vyake vyote kama faini ya kosa.
“Alikubali,
akafilisiwa vitu vyote vikakabidhiwa kwa wazazi wangu ambapo baba
yangu alikuwa mgonjwa hivyo kutokana na kukosa uwezo aliviuza vitu hivyo
kwa ajili ya matibabu na mwishowe akafariki dunia,” alisema.
Mtoto
huyo aliendelea kusimulia kuwa baada ya kuachana na mchungaji huyo kwa
muda mrefu, kuna msichana mmoja mtaani kwao anayejulikana kwa jina la
Asha ambaye alimfuata na kumbembeleza kuwa waende tena kwa mchungaji
huyo, naye akakubali na baada ya kufika huko huku wakiwa wameambatana na
mtoto mwingine wa kiume (17), mchungaji huyo alimfanyia tena mchezo huo
na kumpa fedha huyo msichana hivyo akawa kama yeye ndiye aliyeenda
kuwauza.
“Juzi
hapa mtaani kwetu aliuawa mwizi mmoja, baada ya kuona kile kifo
nilimuita mama yangu na kumwambia natubu maovu yangu ndipo nikaanza
kumwelezea jinsi nilivyorudi tena kwa mchungaji kwa kushawishiwa na huyo
Asha,” alisema mtoto huyo.
Huku
mchungaji huyo akiwa na tuhuma hiyo ya kufanya mchezo huo na mmoja
chumbani na mwingine sebuleni, mwanaume ambaye ni rafiki wa mchungaji
huyo aliyetajwa kwa jina moja la Rahim naye akaingia kwenye mkumbo na
kuendeleza dhambi ya kuwasulubu vijana hao.
Mchungaji
huyo, rafiki yake na Asha, wote waliswekwa nyuma ya nondo za mahabusu
katika Kituo cha Polisi cha Stakishari, Dar na kufunguliwa shitaka namba
STK/RB/13160/2013-ULAWITI wakisubiri kesi yao kuanza kuunguruma.
Wanahabari wetu walifanikiwa kuzungumza na askofu wa mchungaji huyo, Grace Joseph ambaye alikuwa na haya ya kusema:
“Kwa
jinsi ninavyomjua mchungaji wangu siamini kama amefanya kitendo hicho
hivyo tuhuma hizo sikubaliani nazo kabisa ila polisi wanaendelea na
uchunguzi.”
Kwa upande wake mjumbe wa eneo la Kichangani, Majohe, Hawa Kidulu alieleza kuwa
No comments:
Post a Comment