Katika
hali isiyokuwa ya kawaida Hausigeli aitwaye Furaha amenaswa akiwa katika
duka la madawa anauza baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa watu
mbalimbali wakidai mhusika mwenyewe akiwa katika kazi nyingine tofauti
na duka hilo.
Tukio
hilo linadaiwa kufanyika kwa muda mrefu katika duka hilo lililopo
Goroka, Toangoma, Kongowe, Temeke nje kidogo ya Jiji la Dar.Credit:GPL
Akiwa katika famasi akisubiri wateja.
Baada taarifa hizo, ulianza utafiti ambapo iligundulika kuwa mmiliki wa duka hilo anatambulika kwa jina la mama Atu.
Ikadaiwa
kuwa mmiliki huyo ana tabia ya kumuachia duka hilo hausigeli wake
aitwaye Furaha ili auze dawa kwa kubahatisha na mara kadhaa wagonjwa
hupewa dozi ndivyo sivyo.
“Kuna
mwenzetu alikuwa akiugua ugonjwa mwingine, alipofika pale aliandikiwa
dawa za malaria, hali yake ikawa mbaya hadi akakimbizwa hospitalini
kulazwa, tulipomuonya mmiliki hakutusikia,” alisema mmoja wa watu
wanaoijua ishu hiyo kiundani.
Ili kupata ushahidi kamili, Mtu mmoja ilijifanya mgonjwa na kwenda kwenye famasi hiyo kuomba ushauri wa matibabu.
Akimsikiliza mteja.
Hausigeli
huyo alimtajia dawa za typhoid lakini shushushu wetu alimkwepesha na
kumuomba chloroquine ambapo hausigeli huyo alikubali na kutaka kumpa
bila wasiwasi.
Baada ya
kushuhudia hayo alifatwa mwenyekiti wa mtaa huo, Issa Shomari kupitia
mjumbe wake na kufika katika famasi hiyo kujionea hali halisi ambapo
kama ilivyokuwa mwanzo hausigeli huyo alikuwa tayari kutoa huduma.
Baada ya
kikosi kazi kujitambulisha na kumhoji, alikiri kuwa yeye ni mtumishi wa
ndani, ana miaka 16, elimu ya darasa la saba, mwenyeji wa Iringa, huwa
anaachiwa auze na mwajiri wake huku akifunguka kuwa hutoa dawa za
malaria na magonjwa anayoyafahamu.
Akizungumza
kwa mshtuko baada ya kujionea hali halisi, mwenyekiti huyo wa mtaa
alisema kuwa atahakikisha anawasiliana na kamati ya afya ya Wilaya ya
Temeke, Dar ili kuziondoa famasi kama hizo mtaani kwake.
No comments:
Post a Comment