Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, July 22, 2013

ANGALIA PICHA::INASEMEKANA HUYU NDO MTANZANIA MREFU KULIKO WOTEE


Baraka kijana mrefu Tanzania

Inasemekana ni kijana mrefu kuliko wote Tanzania. Kijana huyu (katikati pichani) ambaye anadhaniwa ni mrefu kuliko vijana wote Tanzania anaishi maeneo ya Gongolamboto, Banana jijini Dar es salaam.

 Kijana huyu huwa haonekani sana mitaani, lakini aliingia mjini siku hiyo na kuleta kizaa zaa kikubwa pale alipoibuka mitaa ya Aggrey, Kariakoo. Alikuwa kivutio kwa kila aliyemuona, alifunga mtaa watu wakimshangaa na kumgombania kupiga nae picha. Kila aliyetaka kupiga nae picha alitoa Shilingi elfu moja Tsh. 1000. 

Picha hiyo amepigwa ndani ya Kinyozi (Salon) aliyoingia kupunguza nywele zake na umati wa watu walikuwa nje ya kinyozi huyo kumsubiri atoke. Mpaka sasa hajajulikana jina lake kamili na anafanya nini. 
Hapa Hasheem Thabit alipokutana na Baraka

No comments:

Post a Comment