:
Meneja mpya wa Manchester United David Moyes
amemteua kiungo mkongwe Ryan Giggs kuwa kocha-mchezaji wa timu hiyo ya
Old Trafford leo mchana.
Giggs, 39, ambaye ni kati ya wachezaji
waliotunukiwa nishani nyingi sana katika soka la Uingereza, amekuwa
akifanya mitihani yake ya ukocha na anatarajiwa kupata leseni ya
ukufunzi ya UEFA mwaka kesho.
Mnamo Machi mwaka huu, Giggs
aliongeza mkataba wake wa kuchezea Mashetani Wekundu kwa mwaka mmoja, na
anatarajia kubeba majukumu kamili kama kocha na mchezaji wa kikosi cha
kwanza cha Man U msimu huu. PICHA | AFP
NSSF: Wananchi Waliojiajiri Jiungeni, Jiwekeeni Akiba kwa Kesho Yenye
Uhakika
-
Dar es Salaam, Julai 10, 2026
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umewahimiza wananchi waliojiajiri
nchini kujiunga na kuchangia katika Mfuko huo ili...
9 hours ago


No comments:
Post a Comment