Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, July 4, 2013

Soma Taarifa Maalum Kwa Umma Kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Ruvuma Juu Ya Kuwafikisha mahakamani watumishi 12 wa halmashauri za Mkoa wa Ruvuma kujibu mashtaka mbalimbali ya rushwa chini ya sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Na. 11/2007, sheria ya kanuni ya adhabu Cap. 16 R.E 2002 na sheria ya uhujumu uchumi Cap. 200 R.E 2002 .

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA
S. L. P. 926,
SONGEA – RUVUMA, TANZANIA.

Anwani ya simu: “UCHUNGUZI”
Simu Nambari: 025 2600613
Nambari ya Nukushi: 025 2600663
Barua pepe: rbcruvuma@pccb.go.tz
Simu ya Bure: 113 
--
Katika siku za hivi karibuni, TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma imewafikisha mahakamani watumishi 12 wa halmashauri za Mkoa wa Ruvuma kujibu mashtaka mbalimbali ya rushwa chini ya sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Na. 11/2007, sheria ya kanuni ya adhabu Cap. 16 R.E 2002 na sheria ya uhujumu 
uchumi Cap. 200 R.E 2002 . Washitakiwa waliofikishwa mahakamani ni kama ifuatavyo:

  • ECONOMIC CASE No. 1/2013 – Katika mahakama ya Wilaya ya Mbinga
WASHTAKIWA:

         1. ANTONY SIMON MASHIMBA (65) – EX District Medical Officer
        
 2. FRANCIS FAUSTUS (56) – Coordinator  HIV/AIDS Project - Mbinga
       
  3. JOHN MANDALA (51) – Assistant Accountant – Mbinga District

 
MASHTAKA:

Watuhumiwa walifikishwa mahakamani tarehe 24/04/2013 na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi namba 1/2013 katika mahakama ya Wilaya ya Mbinga. Wameshtakiwa kwa 
 makosa mawili kinyume na kifungu cha 28(1) cha PCCA Na. 11/2007 na kifungu cha 
57(1)  na 60(2) cha sheria ya uhujumu uchumi Cap. 200 R.E 2002.
  • ECONOMIC CASE No. 2/2013 – Katika mahakama ya Wilaya ya Mbinga
WASHTAKIWA:

                        1. PASCHAL J. MAKOYE (36) – Mweka Hazina (W) Mbinga
                       
 2. ROBERT K. MARANDA (42) – Boharia (W) – Mbinga

 
MASHTAKA:
Watuhumiwa walifikishwa mahakamani tarehe 03/05/2013 na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi namba 2/2013 katika mahakama ya Wilaya ya Mbinga. Wameshtakiwa kwa makosa sita kinyume na vifungu vya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na. 11/2007, sheria ya kanuni ya adhabu Cap. 16 R.E 2002 na sheria ya uhujumu uchumi Cap. 200 R.E 2002.
  • ECONOMIC CASE No. 2/2013 – Katika mahakama ya Wilaya ya Namtumbo
MSHTAKIWA:

                        BRUNO N. MFIKWA (47) – EX-Clinical officer, Namtumbo District

MASHTAKA:

Shauri hili lilifikishwa mahakamani tarehe 03/05/2013 na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi namba 2/2013 katika mahakama ya Wilaya ya Namtumbo. Mshitakiwa anakabiliwa na makosa nne kinyume na vifungu vya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na. 11/2007, sheria ya kanuni ya adhabu Cap. 16 R.E 2002 na sheria ya uhujumu uchumi Cap. 200 R.E 2002.
  • CRIMINAL CASE No. 54/2013  – Katika mahakama ya Wilaya ya Tunduru
MSHTAKIWA:

YUSUF SELEMANI MATUMLA (31) – VEO, Kijiji cha Majala –Tunduru

MASHTAKA:

Mtuhumiwa alifikishwa mahakamani tarehe 29/05/2013 na kufunguliwa kesi ya jinai namba 54/2013 katika mahakama ya Wilaya ya Tundurukwa kutenda makosa tisa (9) ya rushwa kinyume na K/F 15 cha PCCA Na. 11/2007.
  • CRIMINAL CASE No. 54/2013  – Katika mahakama ya Wilaya ya Tunduru
MSHTAKIWA:

                     FITINA ADAM MBUYU (38) – VEO, Kijiji cha Tuleane - Tunduru

MASHTAKA:

Mtuhumiwa alifikishwa mahakamani tarehe 14/06/2013 na kufunguliwa kesi ya jinai namba 60/2013 katika mahakama ya Wilaya ya Tundurukwa kutenda kosa la rushwa kinyume na K/F 15 cha PCCA Na. 11/2007.
  • CRIMINAL CASE No. 93/2013  – Katika mahakama ya Hakimu Mkazi Songea
MSHTAKIWA:
                  

   ERNEST IRENEUS HAULE (33) – VEO, Kijiji cha Liganga - Songea

 
MASHTAKA:

Mtuhumiwa alifikishwa mahakamani tarehe 25/06/2013 na kufunguliwa kesi ya jinai namba 93/2013 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Songea kwa kutenda makosa mawili ya rushwa kinyume na vifungu vya 28(1) na 31 vya PCCA Na. 11/2007.

  • CRIMINAL CASE No. 92/2013 – Katika mahakama ya Hakimu Mkazi Songea 
  •  
  • WASHTAKIWA:

         1. BARNABAS B. MTWEVE (54) – HIV/AIDS Coordinator  Songea
       
  2. STEPHEN ANDREW MHANDO (61) – Ex- Ag. DMO Songea
        
 3. MICHAEL JOSEPH SIAJABU (46) – Katibu wa Afya Wilaya Songea
       
  4. CLEMENTINA BEDDDA NGONYANI (71) – Meneja wa ukumbi wa EMAU Peramiho.


MASHTAKA:

Watuhumiwa walifikishwa mahakamani tarehe 25/06/2013 na kufunguliwa kesi ya jinai namba 92/2013 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Songea. Wameshtakiwa kwa makosa kumi na tano (15) kinyume na vifungu vya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na. 11/2007 na sheria ya kanuni ya adhabu Cap. 16 R.E 2002.


IMETOLEWA NA DAUDI MASIKO
MKUU WA TAKUKURU (M) RUVUMA
 

No comments:

Post a Comment