Shekhe Said Juma Makamba
Shekhe Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Said
Juma Makamba amejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa maji yanayohisiwa kuwa
tindikali na watu wasiojulikana juzi usiku akiwa nyumbani kwake jijini
Arusha.
Shekhe
Makamba, ambaye amelazwa katika Wodi ya Majeruhi kwenye Hospitali ya
Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, amejeruhiwa vibaya maeneo ya usoni,
kifuani na mgongoni huku akiendelea na matibabu.
Akizungumza
kwa tabu, shekhe huyo alisema tukio hilo lilitokea saa 5 usiku wa
kuamkia jana nyumbani kwake kwa Mromboo Arusha, wakati akijiandaa kulala
baada ya kutoka kuswali Swala ya Tarawei.
Shekhe
Makamba ambaye pia ni Imamu wa Msikiti wa Sekei mjini Arusha, alisema
baada ya swala hiyo alirejea nyumbani kwake akisindikizwa na vijana
wawili ambao walikuwa wakiswali pamoja na kuingia ndani ya nyumba yake
ili kulala.
Alisema
hata hivyo, kabla ya kulala alikwenda kujisaidia katika choo cha nje na
kwamba wakati akirudi ili aingie ndani akipitia nyuma ya nyumba ghafla
alimuona mtu akiwa amesimama jirani na mlango.
Alieleza kuwa wakati akitaka kumwangalia zaidi alishtukia mtu...
hdg
huyo akiinua mkono na kumwagia maji yaliyompatia maumivu makalisoni na kifuani.
''Wakati
natoka msalani nikipitia uwani kwangu niliona kama mtu ameinama pembeni
yangu wakati najaribu kumsogelea ili nijue ni nani nilihamaki mtu huyo
akinimwagia maji yaliyonisababisha maumivu makali sana yenye asili ya
moto na ngozi kuanza kubabuka,'' alisema shekhe huyo.
Aliongeza
kuwa baada ya tukio hilo alianza kupiga kelele kuomba msaada ambapo
majirani walijitokeza na kumpa msaada wa kumpeleka hospitali, kwa vile
wakati huo macho yake yalikuwa hayaoni na wakati wote alikuwa akilia.
Pamoja na
kujeruhiwa vibaya sehemu za usoni, kifuani na mgongoni, pia ana
majeraha kwenye mikono na machoni na hali yake bado ni mbaya japo
madaktari wanaendelea kumpatia matibabu.
Kaimu
Katibu wa Bakwata Mkoa wa Arusha, Abdallah Masoud akizungumzia tukio
hilo alieleza kushitushwa nalo akisema limefanana na lile la Katibu wa
Bakwata Mkoa wa Arusha, Abdulaziz Jonjo ambaye mwaka jana alilipuliwa
kwa bomu nyumbani kwake akiwa amelala.
Alisema
kuwa matukio hayo yamekuwa yakijirudia huku wahusika wakishindwa kutiwa
mbaroni na kudai kuwa matukio hayo yanahusiana na masuala ya kigaidi.
Aliongeza kuwa pamoja na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, lakini
wamekuwa hawapati matunda ya kukamatwa kwa watuhumiwa ingawa alisema
wanajulikana.
Kwa
upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema
polisi wameanza uchunguzi wa tukio hilo na kwamba taarifa zitatolewa
pindi washukiwa watakapotiwa mbaroni kwani uchunguzi bado unaendelea na
kwamba hakuna mtu anayeshikiliwa hadi sasa.
hdg
No comments:
Post a Comment