Habari kutoka kwa baadhi ya
Watanzania waishio Saint Petersburg, Urusi, ni kwamba Mtanzania
aliyeweka makazi yake mjini hapo kwa muda mrefu Ndg. Shabani Japhari
ameaga dunia kwa kujinyonga.
Akituma ujumbe huo kupitia mtandao
wake wa Facebook, Ndg. Moses Mango, ambaye pia ni mkazi wa muda mrefu wa
Mji huo, alisema ” I hate bringing bad news. Kama wengi mlivyosikia,
ndugu yetu Shabani ametutoka leo asubuhi kwa kujinyonga. Kwa sie wote
hapa, huu ni mzigo mzito sana aliotuachia. Ningeomba wote tuwe pamoja
katika kukamilisha shughuli zote zinazotokana na msiba huu. RIP mrefu",
alimalizia kusema Ndg. Mango.
Shabani alifika Urusi miaka ya 80
kama mwanafunzi, na baada ya kuhitimu masomo yake, alibaki mjini Saint
Petersburg na kuendelea kujihusisha na masuala mbalimbali ya biashara.
Vijana wengi waliokuwa wakifika Urusi ki masomo walimuheshimu na
kumchukulia kama kaka, na wengine kumtaka ushauri katika masuala
mbalimbali kutokana na uzoefu wake wa Mji.
Marehemu Shabani, ameacha mke na
watoto Kandhaa, na dua zetu tunazielekeza kwa familia hiyo, na familia
yake nyingine kubwa, iliyopo Tanzania. Kwa hakika wote tumeshtushwa na
msiba huu, ambao bado umetuacha na maswali mengi, bila majibu.
No comments:
Post a Comment