Boss wa CHELSEA Jose Mourinho amefanya kitendo ambacho sio watu wengi wenye umri wake wanaweza kufanya - mreno huyo amechora tattoo yenye la mkewe kwenye mkono wake.
Mourinho, mwenye miaka 50, alijichora tattoo hiyo baada ya kurejea na timu yake kutoka mashariki ya mbali. Alilipa kiasi cha £80 ili kuchora jina la mkewe 'Matilde Faria' baada ya kuvutiwa na michoro aliyoiona kwa mmoja wa wafanyakazi wa klabu ya Chelsea.Kocha huyo mwenye majivuno alitumia saa nzima kutulia na kuchorwa tattoo hiyo ambayo ndio ya kwanza kwa mchoraji anayefanya shughuli zake karibu na uwanja wa Chelsea uliopo magharibi mwa London.
Mtu aliyemshuhudia kocha alikaririwa akisema kwamba: “Jose alionekana mtu mwenye furaha baada ya kuchora tattoo hiyo.”chanzo shaffih dauda
No comments:
Post a Comment