Watu
wawili ambao ni askari mgambo, wamekimbilia kusikojulikana bado,
wanatafutwa na polisi baada ya kumpiga kwa fimbo kichwani na kumwua
mkulima aliyetambulika kwa jina la Gigwa Malegi (55, Msukuma) na mkazi
wa kijiji cha Iyonyo.
Taarifa
iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi
wa Polisi, Barakael Masaki inasema kuwa mauaji hayo yalitokea tarehe
Mosi Julai, 2013 majira ya saa moja jioni katika kijiji cha Totowe
wilayani Chunya, Mbeya.Taarifa hiyo imewataja watuhumiwa kuwa ni
Focus Fabian na Charles (jina la pili halijafahamika bado).Imeelezwa
kuwa chanzo cha kupigwa na kuuawa marehemu kinatokana na kukutwa
akilisha mifugo (ng'ombe) kaitka eneo oevu kandoni mwa ziwa Rukwa.
Kamanda Masaki ametoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia
sheria mkononi badala yake amewasihi watatue matatizo yao kwa mazungumzo
na kwa kufuata sheria.
Ametoa wito kwa watuhumiwa kujisalimisha mikononi mwa askari mara
moja ama yeyote mwenye taarifa za watuhumiwa, azitoe mara moja katika
mamlaka husika ili hatua za kisheria zichukuliwe.
No comments:
Post a Comment