Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, July 10, 2013

MHANDISI WA MAJI LUDEWA KORTINI KWA UBADHILIFU WA SHILINGI MILIONI 4.2

dsc07978
Na Bazil Makungu Ludewa
TAASISI ya kuzuia na kupambana rushwa wilayani Ludewa (Takukuru) imempandisha kizimbani mhandisi wa maji wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Atanasio Munge kwa makosa ya ubadhilifu wa jumla ya shilingi 4.2 milioni mali ya halmashauri ya wilaya hiyo.
Mbele ya hakimu mkazi mheshimiwa JUMA HASSANI katika mahakama ya mkoa Iringa mwendesha mashtaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Imani Mitume akaiambia mahakama kuwa mshtakiwa anakabililiwa na makosa manne ikiwemo matumizi ya nyaraka kosa linaloangukia kwenye kifungu namba 22 ya sheria ya kuzuiaz na kupambana na rushwa namba 11/2007.
Makosa mengine ni ufujaji na ubadhirifu wa fedha za umma chini ya namba 28(2) sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa na 11 ya mwaka 2007, kosa lingine ni kuibabishia hasara serikali shilingi milioni 4 makosa chini ya kifungu namba 10(1) jedwari la 57(1) na jedwari la 60(2).
Pamoja na mhandisi Atanasio Munge mshtakiwa wa pili ni mfanyabiashara wa mgahawa Videa Kayombo maarufu kama (mama hadija) ambaye jina,saini na mgahawa wake vilitumika kutoa stakadhi zinazoonesha kuwa alitoa huduma hewa ya chakula chenye thamani ya shilingi m.4.2 kwa wananchi wa vijijini katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji wilayani Ludewa inayofadhiriwa na Benki ya dunia.
Akisoma hati ya mashtaka mwendesha mashtaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Imani Mitume alisema watuhumiwa wote wawili walitenda makosa hayo kati ya mwaka 2010 na 2012 na kwamba Vedea Kayombo alitoa risiti za uongo huku akijua kufanya hivyo ni kosa la jinai.
Kufuatia tukio hilo Kamanda wa TAKUKURU wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe Edings Mwakambonja ametoa rai kwa wananchi wilayani humo kutoa ushirikiano na ofisi yake kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa lakini pia akawahimiza kusimamia miradi inayopelekwa na serikali katika maeneo yao.
Mwakambonja pia amewataka watumishi wa umma kuwa waadlilifu katika kazi zao ili kuiepushia serikali hasara na kusababisha kuzorota kwa huduma bora za kijamii jambo linalosababishwa na watumishi wasio na uzalendo na nchi yao.

No comments:

Post a Comment