Umeonaa! Hivi ni kazi yangu
nikimaliza najiajiri. Ndivyo anavyoelekea kusema mwanafunzi Paulina Emmanuel
anayejifunza masuala ya ubunifu wa mavazi na mitindo katika chuo cha VETA Chang’ombe
Dar es Salaam, akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa soko la ajira, mipango na
maendeleo wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Bw. Enock
Kibendela alipotembelea banda a VETA kwenye maonyesho ya SabaSaba, Dar es
Salaam.
Mwanafunzi Ernest Maranya wa
VETA Chang’ombe akitoa maelezo kwa wageni waliotembelea banda la VETA kwenye
maonyesho ya Sabasaba Dar es Salaam akionyesha
kifaa cha elimu ya mfumo wa jua na sayansi ya anga jinsi kinavyofanya kazi
Mkufunzi wa masuala ya hoteli na
Utalii katika chuo cha VETA Njiro, mkoani Arusha Theonestina Raphael akitoa
maelezo kwa askari polisi waliotembelea banda la VETA kwenye maonyesho ya
SabaSaba, Dar es Salaam.
Tukiongeza ufundi kidogo
tutakuwa tumemaliza kazi! Ndivyo anavyoonekana kusema Mkurugenzi wa soko la
ajira, mipango na maendeleo wa VETA, Bw. Enock Kibendela mwenye kofia alipokuwa
akikagua bidhaa za Mamlaka hiyo kwenye maonyesho ya sabasaba, Dar es Salaam.Wengine
katika picha kutoka kushoto ni Mrtibu wa vyuo vya ufundi stadi kanda ya Dar es
Salaam Florence Kapinga na Mwenyekiti wa Kamati ya maonyesho Abdul Mollel na
Afisa Uhusiano wa VETA Dorah Tesha.
Mafunzo kwa watu wenye mahitaji
maalum yanatolewa hivi! Mwalimu Kintu Kilanga mwenye kofia akimueleza
Mkurugenzi wa Soka la ajira, mipango na maendeleo wa VETA Bw. Enock Kibendela
kuhusu mbinu wanazotumia kumfundisha mwanafunzi Range Jackson (kushoto) mwenye
tatizoo la Hyperactive. Hyperactive ni tatizo ambalo linasababisha mtoto kuwa
na uelewa dhaifu wa masuala mbalimbali.
Mwanafunzi Linda Njenje ambaye
ni mlemavu kutoka chuo cha walemavu Usa River mkoani Arusha akionyesha moja ya
bidhaa wanazozalisha chuoni kwao, kwa Mkurugenzi wa soko la ajira, mipango na
maendeleo wa VETA, Bw. Enock Kibendela.
Amani Ibrahimu mjasiriamali
aliyepata mafunzo ya uzalishaji wa bidhaa za ngozi kutoka VETA Dakawa mkoani
Morogoro, akitoa maelezo kuhusu anavyozalisha bidhaa zake kwa Mkurugenzi wa
Soko la ajira, mipango na maendeleo wa VETA Bw. Enock Kibendela kwenye
maonyesho maonyesho ya sabasaba, Dar es Salaam.HABARI NA MROKI MROKI
No comments:
Post a Comment