WAKAZI na wananchi wa Manzese jijini Dar es Salaam, mchana
wa jana ulikuwa mchungu kwao katika fujo zilizosababisha kurushwa kwa
mabomu dhidi ya wafanyabiashara waliokuwa wamejerea katika maeneo
yasiyoruhusiwa.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kuondoka kwa Rais
wa Marekani, Barack Obama, ambaye ziara yake Tanzania ilisababisha
kuhamishwa kwa wafanyabiashara katika maeneo mbalimbali jijini Dar es
Salaam.
Shuhuda wetu alisema kuwa pilika pilika hizo za mabomu ya
Askari Polisi waliokwenda kuhakikisha kuwa wafanyabiashara hao hawarudi
katika eneo la Manzese.
“Hali ilikuwa mbaya mno ambapo pia kurushwa kwa mabomu
kulisababisha kuzua kwa taharuki ya aina yake na baadaye kusababisha
foleni kubwa kwa gari zinazotumia barabara ya Morogoro,” alisema.
Mara baada ya Obama kurudi kwao Marekani, wafanyabiashara
ndogondogo wamerudi tena katika vijiwe vyao kuendelea na biashara zao,
ambapo serikali ya jiji imesema itahakikisha kuwa watu hao hawarudi tena
katika maeneo yasiyoruhusiwa.
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Mecky Sadick, alisema jana kuwa
suala la kuwabana wafanyabiashara hao wasirudi katika maeneo
yasiyoruhusiwa ni jambo la lazima pamoja na kulitunza jiji kutokana na
uchafu.
No comments:
Post a Comment