KUSHOTO: Mandla Mandela. KULIA: Msafara wa maofisa wa polisi pamoja na gari la kubebea maiti wakielekea kusaka miili nyumbani kwa Mandla huko Mvezo. |
Polisi wa
Afrika Kusini wamevamia nyumbani kwa mjukuu wa Nelson Mandela kusaka
miili mitatu anayodaiwa kuihamisha kinyume cha sheria.
Hii
imekuja baada ya Mandla Mandela juzi kushindwa kesi mahakamani dhidi ya
ndugu 16 wa familia yake ambao wanamtuhumu kwa kuhamisha miili hiyo ya
watoto watatu wa rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini bila idhini yao.
Mahakama ya Mthatha iliamua kwamba mabaki hayo yarejeshwe katika eneo ya maziko la familia hiyo hadi kufikia juzi Saa 9 alasiri.
Askari wa Mahakama walivamia milango ya kuingia
nyumbani kwake huko Jimbo la Eastern Cape nchini Afrika Kusini wakiwa na
mashoka kabla ya maofisa wa polisi kufukua ardhini kusaka miili hiyo.
Magari matatu ya kubebea maiti mazikoni pia yalionekana kwenye eneo
hilo, gazeti la Eyewitness News la Afrika Kusini liliripoti.
Familia hiyo ilimburuta Mandla mahakamani baada ya kuzika upya mabaki ya miili katika eneo lake alikozaliwa la Mvezo mwaka 2011.
Ndugu wa Mandela walidai kwamba Mandla hakuwa na ruhusa au hata kuwataarifu wanafamilia wakati akifanya maamuzi hayo.
Ndugu wa Mandla wamesema kwamba nafasi yake kama chifu wa kijiji hicho sasa iko hatarini
No comments:
Post a Comment