Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, July 16, 2013

TAARIFA KWAVYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUHOJIWA KWA MBOWE


Advera-SensoAdvera Senso-SSP Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Leo tarehe 15 Julai, 2013 majira ya mchana, mwenyekiti wa chama cha CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe amejisalimisha Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, kufuatia tuhuma mbalimbali ambazo zimekuwa zikimkabili zikiwemo kauli za uchochezi ambazo amekuwa akizitoa dhidi ya Jeshi la Polisi, Vyombo Vingine vya dola na Serikali kwa ujumla.
Jeshi la Polisi nchini, linaendelea kumhoji Mhe. Mbowe juu ya kauli hizo ambazo zimekuwa na mlengo wa uchochezi na kuijengea jamii taswira hasi juu ya vyombo vya ulinzi na usalama na kuwafanya wananchi kuwa na hofu.
Aidha, uchunguzi wa kina unaendelea na pindi itakapothibitika kuhusika kwake ama mtu mwingine yeyote kutoka ndani au nje ya chama cha CHADEMA hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kufikishwa mahakamani.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

No comments:

Post a Comment