Asubuhi ya leo kulikuwa na press conference ya Tamasha la matumaini iliyofanyika kwenye hotel ya Atriums maeneo ya kijitonyama, Binafsi mimi na wasanii wengine wa Bongo Flavour,Bongo Movie,wabunge, pamoja na wanamasumbwi watakaoshiriki walikuwepo pia kwenye mkutano huo na waandishi wa habari....!!Nia ni kuzungumzia mchango wetu na wa kila mmoja kwenye Tamasha la Matumaini litakalofanyika tarehe 7.7.2013 kwenye uwanja wa Taifa.... Madhumuni ya Tamasha ili ni kama jina linavyojieleza, madhumuni ya kwanza ya tamasha ili ni kurejesha matumaini miongoni mwa watanzania ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema ; 'Licha ya tofauti zetu za kidini na kiitikadi,lakini sisi sote ni Watanzania....!!Aidha madhumuni ya pili ya tamasha hili ni kuchangia mfuko wa elimu wa Tanzania,ambayo tangu mwaka jana imekuwa katika kampeni ya kukusanya fedha kwaajili ya ujenzi wa mabweni ya wasichana katika shule za sekondari nchini..Sehemu ya faida itakayopatikana katika tamasha ili zitawezesha mfuko huo wa elimu ya juu... Burudani mbalimabli zitakuwepo siku hiyo ni kuanzia muziki wa dansi, muziki wa taarabu,muziki wa injili,muziki wa kizazi kipya, soka na ndondi....!! Upande wa soka kutakuwa na mechi kati ya wabunge wa Bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania baina ya wabunge wa simba na yanga...! Katika ndondi atakuwepo msanii wa Bongo movie Jacquline wolper atazichapa na Mbunge wa chadema Halima Mdee uku Mbunge wa Chadema kwa wanaume akizichapa na Msanii wa bongo movie vicent kigosi maarufu kama Ray...!! Katika kupendezesha usiku wa matumaini kutakuwa Pambano la kimuziki wa Kimataifa kati ya kenya na Tanzania,kutoka Tanzania tutawakilishwa na Rais wa wasafi Diamond Platnumz na kutoka Kenya watawakilishwa na Prezzo, katika mpambano wa Ngumi za Kimataifa kati ya Kenya na watanzania kati ya Thomas Masharia wa Tanzania atazipiga na Bondia Patrick amote kutoka kenya na Thomas Miyeyusho atapanda ulingoni na Shadrack Muchanje kutoka kenya mabondia hawa watagombea ngao ya Amani ya Afrika Mashariki...!! Siku hiyo viingilio vitakuwa 5,000/= ndio kiingilio cha chini kuliko vyote viti vya mzunguruko wa juu na wakati Tsh 10,000/= utakuwa vitii vya orange na bluu na V.I.P iatakuwa kwa Tsh 20,000/= Tamasha litaanza kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 6 usiku
Zifuatazo ni Picha na waandishi tofauti wa Habari...!! |
No comments:
Post a Comment