Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, July 7, 2013

TAZAMA PICHA ZA KILICHOJIRI KATIKA UTOAJI WA TUZO ZA ZIFF, AMBAPO LULU ALIJISHINDIA TUZO




Amili Shivji
Amili Shivji mtayarishaji wa filamu ya Shoeshine.
TAMASHA la kimataifa la filamu nchi za Majahazi Zanzibar Intertainational Film Festival (ZIFF) limeendelea leo na kutoa tuzo kwa filamu zilizoshinda kupitia tuzo mbalimbali katika vipengere tofauti tofauti, huku afrika ya Kusini akijizolea tuzo nyingi, lakini pia mabadiliko makubwa yamefanyika baada ya filamu nyingi au zilizotemewa kutoka Bongo Movie kutoka kapa.

.
Kombo
Mwenyekiti wa ZIFF akiongea katika tuzo usiku jumamosi.
Washindi wa tuzo
Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi.
Tuzo ya kwanza kutolewa ilikuwa Verona (African Film Festival of Verona) nyingine ni Gangster project ya Teboho Edkins (South Africa) , East African Talent Award ni Kivuto kutoka (Rwanda) ya Poupoune Sesonga ambaye amepata– 1000 USD, filamu ya Ni Sisi ya Nick Reding kutoka Kenya, Little One ya Darrell Roodt wa South Africa.
.
Ziff
Tamasha la filamu nchi za Majahazi
washindi wa ziff katika picha ya pamoja na viongozi
washindi wa ziff katika picha ya pamoja na viongozi
TUZO ZA ZUKU BONGO MOVIE
Ambazo ni kitengo cha kipekee ziliandika historia baada ya kuwaibua waigizaji wasio na majina kabisa mwigizaji bora wa kiume kwa filamu ya Kiswahili Bond bin Suleiman ‘Boby’ katika filamu ya Lover’s Island, mwigizaji bora wa kike ni Elizabeth Michael ‘Linda’ kupitia filamu ya Woman of Principal huku Muongozaji
Bora akiwa ni Bond Bin Suleiman filamu ya Lover’s Island, Filamu Bora ni Lover’s Island ya Bon Bin Suleiman na filamu ilishinda kama chaguo la watu (Peoples Choice Awards) ni Shoeshine ya Amil Shivji kutoka Tanzania.
Tuzo ya OUSMANE SEMBENE ambayo mshindi upata – 5000 USD filamu iliyoshinda ni NO PROBLEM! SIX MONTHS WITH BAREFOOT GRANDMAMAS Iliyoandaliwa na Yasmin Kidwa kutoka n(India.)
SAVE THE CHILDREN Award Tuzo kwa ulinzi wa watoto mshindi ni Little One Darrell Roodt kutoka South Africa.
TUZO ZA ZIFF (ZIFF AWARDS) 2012/ 2013. Golden Dhow ni Golchereh ya Vahid Mousaian kutoka Iran, tuzo za Silver dhow: Ni Ni Sisi ya Nick Reding kutoka Kenya, filamu Bora Afrika Mashariki ni Nairobi Half Life Tosh Gitonga kutoka Kenya, na makala Bora ni No Problem: 6 Months In The Barefoot Grandmother ya Yasmin Kidwai wa India.
Amil Shivji
Amil Shivji mshindi wa tuzo ya Peoples choice.
Filamu fupi fupi ni :Sabbat El Aïd My Shoes ya Anis Lassoued kutoka Tunisia, tuzo nyingine maalumu ilikwenda kwa kijana wa kimasai Peter Biella filamu The Chairman and the Lions Marekani na Tanzania ,Special mention: Fluorescent Sin , Amirah Tajdin, (Kenya) Adamt , Zelalem Woldemariam, (Ethiopia) Hasaki ya suda, Cedric Ido, (France/Burkina Faso)
Tuzo ya kutukuka (Lifetime Achievement Award) alitunikiwa Prof. Abdul Sherif , Tuzo ya Heshima ya msanii Bi. Kidude iliyopewa jina la Chairman’s Bi Kidude Award ilitunikiwa filamu ya CRUSH iliyotengenezwa na Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar Es Salaam Issa Mbura, filamu iliyoelezea maisha halisi ya vyuo vikuu nchini na imeigizwa na wanafunzi pamoja na wasanii kama Mzee Chilo, Masinde na wasanii wengine.NA BONGOCLAN TZ


No comments:

Post a Comment