Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, July 14, 2013

Timu ya Azam Academy imefanikiwa kuingia fainali ya Mashindano ya Kombe la Rolling Stone 2013


Kutoka Arusha: Timu ya Azam Academy imefanikiwa kuingia fainali ya Mashindano ya Kombe la Rolling Stone 2013 baada ya kuwatoa Coastal Union B' kwa penati ya 5-4 kwenye mchezo wa nusu fainali iliyochezwa leo asubuhi Uwanja wa General Tyre, kabla ye penati mechi ilimalizika kwa timu zote kutoka suluhu (0-0)!

Kabla ya penati mechi timu hizo zilimaliza muda wa kawaida zikiwa hazijafungana (0-0).

Mikwaju ya penati ya Azam Academy ilifungwa na Abdul Mgaya, Ismail Adam Gambo, Kelvin Friday, Adam Shoba na Abdalah Shirazi

Azam Academy itakutana na Eagle ya Tanga katika mchezo wa fainali itakayochezwa siku ya Jumanne, timu hizo zinakutana kwa mara ya pili baada ya kucheza hatua ya makundi ambapo Azam Academy waliifunga Eagle 3-0.

Pongezi kwa wachezaji wa Azam Academy,

No comments:

Post a Comment