Na Baraka Mpenja kwa Msaada wa Sportsmail.com
Kocha
wa Mabingwa wa soka nchini England, Manchester United, David Moyes
ameweka wazi mpango wake wa kutafuta kiungo mshambuliaji mpya, huku
akithibitisha kuwa mshambuliaji wake hatari, raia wa Uholanzi, Robin Van
Persie atakuwa mshambulaiji wake namba moja msimu ujao na kuleta hofu
kubwa juu ya hatima ya baadaye ya Wayne Mark Rooney, dimbani Old
Trafford.
Inafahamika
kuwa Moyes anataka kumleta kiungo mshambuliaji wa FC Barcelona, Cesc
Fabregas mwenye uwezo na ujuzi wa hali ya juu kumudu nafasi yake na kama
dili litafanikiwa basi nafasi ya Rooney itakuwa mahali pabaya sana.
Katika
mfumo wa kocha mpya wa United, inafahamika wazi kuwa nyota raia wa
Japan, Shinji Kagawa, atatumika kama namba kumi nyuma ya Robin Van
Persie, hivyo hali hiyo kumshangaza Rooney wapi atacheza.
Lakini katika mahojiano aliyofanya Asia, Moyes alisema bado anatamani
kumbakisha Rooney, ambaye amerejea England baada ya kupata majereha ya
nyama za paja. Pia alisisitiza kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 27,
bado ana umuhimu mkubwa sana katika kikosi chake.
Hata
hivyo, Mkurugenzi mkuu wa Manchester United, Ed Woodward alisisitiza
kuwa klabu hiyo haina mpango wa haraka kuzungumza na Rooney juu ya
kuongeza mkataba wake kwani bado ana miaka miwili zaidi, lakini nyota
huyo anaonekana kuwa na nia ya dhati kutaka kuihama klabu hiyo.
Wakati
huo huo Jembe la United, Robin Van Persie limewashawasili kujiunga na
wenzao katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu nchini
England ambapo United watakuwa wanatetea taji lao walilotwaa msimu
uliopita.
Karudi kazini: Robin van Persie amerudi na kujiunga na Manchester United katika ziara yao Sydney
Maisha ya Rooney ya baadaye katika klabu yake ya United bado haijulikani
Moyes amesema atamhitaji Rooney endapo tu Robin Van Persie atakuwa majeruhi
Jembe hilo: Robin van Persie akiwasili kujiunga na Manchester United katika hoteli Sydney
Moyes
ameweka wazi kuwa msimu ujao bado jembe lake, ARV litatumika kutetea
ubingwa wao, na Rooney atasubiri mpaka akipata majeraha
Meneno
hayo ya busara kwa upande wa pili: Wakati Moyes akisema hayo, bosi wa
Chelsea, Jose Mourinho ameweka wazi nia yake ya kumhitaji Rooney, lakini
Moyes alitangaza kuwa nyota huyo hauzwi
No comments:
Post a Comment