Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, August 21, 2013

AJALI YA LORI NA GARI NDOGO MOROGORO


Gari Aina ya Prado tz ikiwa imepata ajali kwa kugongwa la lori la mizigo jana usiku Maeneo ya Nane Mkoani Morogoro.Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo ni kwamba Chanzo Cha Ajali hiyo ni Uzembe wa Dereva wa Gari ndogo aina ya Prado iliingia barabara kuu bila kuangalia pande zote kama kuna gari nyingine na ndipo alipoingia na kukutana la Lori La Mizigo likiwa kwenye Mwendo kasi na ndipo lilipoligonga gari hilo.Kwenye Gari Dogo alikuwa dereva Mwenyewe Hakuna Mtu Aliyepoteza maisha.
Mashuhuda wa ajali hiyo wakiwa eneo la tukio wakiliangalia gari hilo lililopata ajali Eneo la Nane nane Mkoa wa Morogoro jana usiku.
Picha ya gari hilo mara baada ya kuondolewa eneo la tukio na hivi ndiyo lilivyoharibika baada ya Ajali Hiyo
Askari Polisi wakiwa Eneo la tukio muda Mfupi Mara baada ya ajali hiyo kutokea
Askari wa usalama barabarani akiwa eneo la tukio hapa akilikagua muda mfupi mara baada ya kutokea ajali hiyo Mkoani Morogoro
Lori lililopata ajali hiyo likiwa limeharibika.Picha na MATUKIO NAMICHAPO BLOG

No comments:

Post a Comment