Fainali
za Dunia za Miss Utalii 2013 (Miss Tourism World 2013),zitafanyika
nchini Equatorial Guinea, trehe 2 ,Oktoba 2013. Fainali za Dunia mwaka
huu zitashirikisha zaidi ya nchi 100 kutoa dunia nzima ikiwemo
Tanzania.
Katika
fainali hizo za Dunia ambazo Tanzania itakuwa inashiriki kwa mara ya
tano ,itawakilishwa na mshindi wa taji la Taifa la Miss Utalii Tanzania
2013, Hadija Saidi Juma (Pichani), ambaye pia ni Miss Utalii Morogoro
2013. Hadija Saidi Juma, ambaye alitwaa taji la Taifa baada ya
kuwashinda warembo wengine 29 kutoka mikoa yote ya Tanzania na Vyuo
Vikuu katika fainali za Taifa , zilizo fanyika tarehe 9-5-2013 katika
uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga, ataondoka nchini tarehe 28-10-2013.
Miss
Utalii Tanzania imeijengea heshima kubwa Tanzania, sio kwa kuwa ya
kwanza kutwaa taji la duni nchini tu,bali pia kwa kushinda mataji katika
fainali zote za dunia tulizo shiriki, ambapo hadi sasa tunashikilia
mataji manne ya Dunia.Mataji
hayo na nchi yaliko fanyika katika mabano ni pamoja na Miss Tourism
World 2005 –Africa (Zimbabwe), Miss Tourism World 2006 – SADEC (China
Taipei), Miss Tourism Model Of The World 2006 – Personality (Tanzania),
Miss Tourism World 2007 – Africa (Uturuki), Miss Africa 2006- 1st Runner
Up na Miss Freedom Of The World 2013- Model.
Maandalizi
ya kumwandaa Miss Utalii Tanzania 2013, kwaajili ya kushinda taji la
dunia,yanaendelea vizuri ,ili aweze kulinda heshima ya Tanzania na
kuvuka rekodi ya warembo waliotangulia yanaendelea vizuri. Ambapo ili
kuhakikisha ushiriki wake katika mashindano hayo ya dunia unakuwa na
manufaa ya kutangaza Utalii wa Tanzania kimataifa, tumesha peleka maombi
maalum Katika mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na mamlaka ya Hifadhi za
Taifa ziweze kudhamini ushiriki huo na kufanikisha zaidi maandalizi.
Tofauti
na mashindano mengine, washiriki wote wa fainali hizo za dunia watapewa
fulsa maalum ya kutangaza utalii na utamaduni wan chi zao kupetia
vyombo mbalimbali vya habari duniani, jukwaani na nje ya jukwaa.Hii
itkuwa ni fulsa nyingine ya pekee kwa Tanzania,TANAPA na Ngorongoro
Crater kutangaza Hifadhi na vivutio vya utalii vya Tanzania kimataifa,
kupitia Miss Utalii Tanzania 2013 katika mashindano hayo.
0789 343435 -Mwenyekiti Mtendaji
Miss Tourism Tanzania Organization / Africa Tourism Promotion Center
Na Tabianchi
No comments:
Post a Comment