Dereva
wa boda boda Cheni Abed akiwa chini baada ya pikipiki yake kugonga na
baiskeli kwenye makutano ya barabara za Mafisa,Kichangani
Dereva wa
boda boda Aliyejulikana kwa jina Bw Cheni Abed kufariki dunia baada ya
kugongana na baiskeli huku dereva wa baiskeli hiyo ambaye pia alimpakia
mwanaye wakiwa salama salmini.
Cheni
ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Mchuma kata ya Kichangani mkoani hapa
alipoteza maisha baada ya kugongana na baiskeli hiyo na kuangukia
kichwa kwenye makutano ya barabara za Msamvu,Mafisa,Mwembesongo huku
dereva wa baiskel hiyo ambaye alimpakia mwanye wakisalimika kwenye tukio
hilo.
Umati wa watu ukishuhudi tukio hilo la aina yake
Kufuatia
mazingira ya tukio hilo familia ya dereva boda boda huyo iliamua
kusafiri hadi wilaya ya mvomero kwenda kwa mganga wa kienyeji kuchunguza
mazingira ya kifo hicho ambapo Sangoma Hamis Masai mkazi wa kijiji cha
Changarawe kata ya Mzumbe Wilaya ya Mvomero mkoani hapa alimueleza baba
wa mzazi wa marehemu huyo Bw Abed Shabani kwamba mama yake mzazi ndiye
alimuua mjukuu wake huyo kwa kumchukua msukule na kwamba Sangoma huyo
alimhakikishia Mzee Shabani kwamba alikuwa na uwezo wa kumrejesha dunia
mwanye huyo aliekuwa nguvu muhimu kwenye familia hiyo.
Kufutia
kauli hiyo Mzee Shabani aliludi Morogoro mjini na kusitisha mazishi ya
kijana wake kwa siku nne akisubiri mganga huyo amfufue, kufuatia taarifa
hizo majirani ambao yatari walishaanza kutoa msaada wa kuchimba kaburi
na kuchanga michango ya mtaa walizuiwa kufanya shughuri hizo kwa maelezo
kwamba Cheni angefufuliwa.
Habari
za kufufuka kwa boda boda huyo zilizagaa kwa kasi kubwa kama kile
kimbunga cha sunami na kwamba siku ya nne aliyohadi mganga huyo kumfufua
boda boda huyo ilipofika umati wa watu kutoka kona zote za mji wa
morogoro walifuka nyumbani kwa mzee Shabani akiwemo wmandishi wa habari
hizi kwa lengo akushuhida maajabu hayo. Na Dustan Shekidele..
Familia
hiyo na wananchi hao walisubiri toka saa mbili asubuhi hadi saa moja
usiku bila kushuhudi boda boda huyo akifufu liwa na kwamba Sangoma huyo
alipoulizwa na familia hiyo alidai kwamba kuna mashariti yalivunjwa na
familia hiyo hivyo asingewe tena kumfufua marehemu wao na kwamba baada
ya kauli hiyo watu walitawanyika na kurudi siku iliyofuta kumzika boda
boda huyo.
Katika
mazishi hayio kuliibuka mambo kadhaa ambapo miongoni mwa mwambo hayo ni
mashekhe wote wa kata ya kichanga kugoma kwenda kumsalimi marehmu huyo
wakiitaka familia hiyo kwenda kumwita mganga huyo wa kiennyeji
wanayemuami aje kumsalia marehemu wao.
Familia
hiyo baada ya kuona viongozi hao wa dini wamevuta 'Hend Breck' wameamu
kukodi boda boda na kwenda kumfuta shekh Mageta ambaye ana undugu na
familia hiyo na kwamba kwenye mawaidha yake Shekh Mageta akiipiga madogo
familia hiyo kwa kuabudu mamboya kishirikina.
"Nimepata
ahabari mashekh wenzangu wa eneo hili wamesusia kuja kwenye msiba huuu
kwa mambo yetu ya kijinga ya kuabudu ushirikina kijana wetu amekufa kwa
ajari na amenguaki kiichwa damu mwingi zimetoka leo mnaenda kuangua kwa
mganga kuchunguza kifo chake na mnadanganywa eti mganga huyo naweza
kumfufua mtu mbona ameshinwa kumfufua naomba sikunyingine msiludia jambo
hili" alisema Shekhe mageta kwwnye mawaidha yake
Mwenyekitim
wa taa huo wa chuma Bw Nathanael Chacha ambaye alikiri kupokea taarifa
za familia hiyo kumfufua kijana wao alimu kuwaambia wajumbe wake
waliokuwa kwenye zoezi la kuchanga pesa za pole kuacha zoezi hilo
Jambo
la tatu lililojiri kwenye msiba huo ni kwamba kwenye acouti ya simu ya
marehmu kulikutwa pesa taslimu shilingi laki sita na kwamba dada za
marehmu walihangaika kuzitoa pesa hizo bila mafanikia baada ya kushindw
akuitambua namba ya siri ya marehmu huyo licha ya kujari kuweka namba ya
siri ya mwaka wa kuzaliwa wa maremu huyo.
Baba
mzaza wa marembu Mzee Abed Shabani alipohojiwa na mtandao huu alikiri
simu ya mwanayen huyo kuwa na kiasi hicho cha fedha na kuda kwamba
wanashindw akuzitoa baada ya kutoitambua namba ya siri,habari ambazo
mtandao huu umezinasa zilidai kwamba mchumba wa boda boda huyo ambaye
ameza naye mtoto mmoja ndiye pekee nayejua namba za siri za simu ya
mpenzi wake na kwamba kuna habari zinadai kwamba wifi zake kwa sasa
wamemficha jambo hilo naye amedai kwamba kamwe hawezi kuwataji namba
hizo za siri mapka atakapohakikishiwa mgeno wa fedha hizo yeye na mtoto
wake.
mwendezo
wa tukio hili kwa maaba ya picha za mazishi utawajia kesho hivyo
usikose kutemebea mtandao huu kujua mengi kujuu ya tukio hili ikiwemo ya
bibi huyo wa marehmu aliyetumia uchawi naye kufariki duni kwa Sangoma
huyo
Polisi
wakimpaki kwenye gari boda boda huyo kwa lengo la kuhospital ambayo
kabla ya kufika hospital boda boda huyo alifika njiani
Mungu ni mkubwa dereva wa baiskeli hiyo alimpakia mwanae huyu ambaye hakuumia popote kwenye ajari hiyo
Gari ya polisi akielekea hospita ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.
No comments:
Post a Comment