JESHI
la Polisi Kenya wapo katika uchunguza baada ya kichwa cha mtu aliyeuawa
kiliwa kimewekwa nje ya afisi ya mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya
polisi Johnston Kavuludi jijini Nairobi.Kifurushi kimefungwa kwa karatasi ya plastiki, vilevile kilikuwa na mikono miwli ya binadamu iliyojaa damu.
kando ya kifurishi hicho kulikuwa na ilaani iliyoandiskwa ''Kavuludi wewe ndiye utakayefuata''.Tangu
uteuzi wake, kamishna huyo ameongoza harakati za kujaribu kuifanyia
marekebisho idara ya polisi ambayo inadaiwa kuwa fisadi zaidi Afrika
Mashariki.
Kwa
mujibu wa idara ya polisi, hakuna mshukiwa aliyekamatwa kauhusiana na
tukio hilo na kuwa bado wangali wanachunguza mwili huo ulikuwa wa nani.
Katika
miezi ya hivi karibuni kumekuwa na uhasama kati ya tume hiyo
inayoongozwa na Kavuludi na ofisi ya mkuu wa polisi, huku zikilumbana
kuhusu nani ana madaraka ya kuliendesha idara hiyo.
No comments:
Post a Comment