Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, August 8, 2013

ANGALIA PICHA YA JENGO REFU KULIKO YOTE DUNIANI





jengo refu kuliko yote duniani na kulitaja Sky City One ambalo bado linajengwa nchini China kama ndio jengo refu kuliko yote duniani. Baadhi ya watu wangu wa nguvu hawakukubaliana na habari ile na kusema kwamba Kingdom Tower linalojengwa Jeddah Saudi Arabia ndiyo jengo refu zaidi duniani.
Kutokana na hilo napenda kuwajulisha mambo kadhaa ambayo ni vizuri wote tukayajua kuhusu ishu ya majengo marefu duniani. Kitu cha kwanza napenda kuwapa habari kwamba jengo la Kingdom Tower halijulikani litakuwa na urefu gani hadi sasa. Mwanzoni lilitolewa wazo kuhusu ujenzi wa jengo hili liwe na urefu wa kilomita 1.6, lakini licha ya mawazo hayo kutolewa bado halikuchorwa kabisa katika huo urefu.  Kutokana na eneo ambalo linajengwa hili jengo, wataalamu walishauri kutokana na hali yaki jiolojia halitakiwi kujengwa kwa urefu huo.
Hadi sasa hivi jengo linajengwa lakini haijawekwa wazi litakuwa na urefu gani kama ilivyokuwa kwa Burj Khalifa ambalo lipo Dubai. Huu hapa ni shahidi kutoka kwenye wikipedia, moja kati ya sehemu za uhakika sana za kupata maelezo ya kitu chochote kile.
tower
Watu wangu wa nguvu, topic ya jengo lipi ni refu inaleta utata hadi kwenye nchi za wenzetu. Wadadisi wengi wanauliza jengo refu duniani tulipate kwa kuzingatia vigezo gani?. Jiulize na wewe, ili jengo liwekwe kwenye list ya majengo marefu linatakiwa liwe kwenye hali gani,haya ni baadhi ya maswali ambayo yanaibuka sana kwenye hii ishu ya jengo refu.


    Je, jengo refu duniani lazima liwe tayari limekamilika
    Jengo ambalo bado linajengwa linaweza kuingia kwenye listi
    Jengo linatakiwa kuwa tayari limeshakalika,limefunguliwa na linatumika
    Majengo yanayoanzia chini ya maji hasa baharini, ile sehemu ya chini ya maji ihusishwe kwenye urefu au tuanzie kwenye usawa wa maji. Hii inahusisha sana hotel ya Burj Al Arab na mengine yaliyojengwa baharini
    Urefu wa jengo uhesabiwe inapoishia vyumba au hadi tower ya juu ihusike. Kama ulikuwa hujui majengo mengi yana towers kwa juu lakini vyumba vinaishia chini kidogo ya iyo tower

Hayo maswali yamewafanya wachunguzi wengi kuja na list zao wenyewe, lakini ikiwa wahusika wa jengo wamesema rasmi jengo hili lina urefu flani. Basi mara nyingi linahusishwa kwenye list ya majengo marefu duniani. Kitu cha mwisho ni angalizo kwa kila mtandao unaosoma, hakikisha ni wakuaminika kwa kila habari unayosoma. Siku hizi mtandao kila mtu ana uhuru nao na maelezo mengi haya hoja za kutosha kuyatetea maelezo hayo. Natumaini tumeelewana lakini nakubali kwamba kuna kuchanganyana sana kuhusu hii ishu ya jengo lipi ni refu duniani hasa linapokuja swala la sifa zilizotumika kutengeneza hiyo listi

No comments:

Post a Comment