Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, August 8, 2013

Kenya yapata channel mpya ya TV ambayo wasanii watafaidika nayo kimapato.Kampuni ya ving’amuzi ya StartTimes Kenya imeanzisha channel mpya inaitwa Triple P ambayo itakuwa inahusika na kurusha material ya entertainment tu kutoka Kenya kwa masaa 24. Triple P itapewa leseni rasmi na Music Copyright Society of Kenya (MCSK) kucheza kazi za wasanii wa Kenya kwenye channel ya Triple P ambapo leseni hiyo watailipia kila mwaka. Kutokana na kulipia  leseni hiyo, kampuni ya StarTimes pia inakuwa na nafasi ya kutoa na ruhusa au kibali cha wamiliki wa maeneo kama supermarket,banks,malls,restaurant na sehemu kama hizo za wazi kuonyesha channel hii kwa malipo maalum. Sehemu hizi channel hii itakuwa inaoneka kwa jamii nzima bure, ambapo watu wengine watakuwa hawajalipia hiyo channel lakini wanaangalia. Malipo haya maalum  kwa wamiliki wa eneo husika yanatokana na sababu kama hii.
Mapato haya yote yataweza kuwafikia wasanii kutokana na leseni inayolipiwa kila mwaka na kampuni ya Startimes kwenda Music Copyright Society of Kenya (MCSK). Triple P itapatikana kwenye package zote za StarTimesLaunch_7

No comments:

Post a Comment