Kifaa hicho kikionyeshwa kwa wananchi, waumini na wanahabari.Kifaa cha TMA kikitolewa katika transfoma.
Watu wa dharura wakiondoka baada ya kubaini kuwa ni kifaa cha TMA.
(Jumapili) hali ya taharuki ilizuka kwa waumini wa Kanisa la KKKT
Usharika wa Kijitonyama wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam baada
ya kuonekana kifaa cha Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
kilichosadikiwa kuwa bomu.
Kifaa hicho ambacho kilifungwa katika boksi kilikutwa juu ya transfoma umbali wa takribani meta 20 kutoka nje ya kanisa hilo.
Akizungumza
mbele ya waandishi wa habari jana, Mtabiri Mwandamizi wa TMA, Agustine
Kanemba alisema kifaa hicho huwa kinarushwa kila siku kwenda angani kwa
urefu wa kilometa 55,000 kikiwa kimeambatana na puto.
Alisema
kikifika huko puto hupasuka na kusababisha kifaa hicho kudondoka chini
jambo ambalo linasababisha wao kupata taarifa za hali ya hewa ya anga
baada ya hatua hiyo.
No comments:
Post a Comment