Basi la Bedui lenye namba za usajili T 273
ACX jana lilipinduka katika makutano ya barabara ya Tabora na ile
iendayo Bukoba maeneo ya Nyihongo, Kahama mkoani Shinyanga. Watu 40
wamejeruhiwa katika ajali hiyo ambayo chanzo chake inadaiwa kuwa ni
dereva kushindwa kukata kona iliyopo katika makutano hayo. Basi hilo
lilikuwa likitoka Kahama kuelekea Tabora na kwa mujibu wa taarifa kutoka
kwa Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama, hakuna
abiria aliyepoteza maisha katika ajali hiyo, japo majeruhi sita
walioumia sana wamepelekwa katika hospitali ya Bugando mkoani Mwanza kwa
matibabu zaidi.
(Picha na Mdau Yohana Jackson)
No comments:
Post a Comment