Msanii huyu amesema kuwa, amekuwa katika ugomvi wa hapa na pale na baba mwenye nyumba wake ambaye Sehemu ya nyumba yake ndiyo inatumika kama Bar ya Dudu Baya – Mambaz Pub.
Dudu
Baya amefafanua kuwa katika kipindi cha nyuma wakati Dudu baya yupo
safarini, Mwenye nyumba huyu aliwahi kuvamia baa hii na kungoa feni
pamoja na uharibifi mwingine ishu ambayo Dudu Baya kupitia Mpenzi
wake aliiripoti polisi na kumfungulia kesi ambayo inaendelea mpaka
sasa.
Kwa
mujibu wa Dudu Baya, kilichosababisha mpaka yeye akaenda polisi
mwishoni mwa wiki ni kutokana na Kesi ya kizushi ambayo mwenye nyumba
huyu amemfungulia ili kupunguza makali ya kesi yake inayomkabili hivi
sasa.
Siku
ya leo Polisi wameripiotiwa kufika eneo la tukio kuchunguza Uharibifi
wa kuchoma moto ambao Dudu Baya aliripotiwa kuufanya pamoja na
kuhojiana na pande zote mbili ili kuweza kujua hatua muafaka ya
kuchukua.SOURCE SAMMISAGO.COM
No comments:
Post a Comment