Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Klabu
ya Roma inayocheza ligi kuu nchini Italia, Seria A, imekamilisha
uhamisho wa mshambuliaji wa Arsenal yenye makazi yake kaskazini mwa
London, Gervinho kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni saba.
Nyota
huyo raia wa Ivory Coast alishindwa kuonesha makali yake tangu ajiunge
na Arsenal mnamo mwaka 2011 na sasa anatarajia kufanya kazi na kocha wa
Roma, Rudi Garcia, ambaye ni kocha wake wa zamani akiwa klabu ya Lille
ya Ufaransa, na pengine ataonesha cheche zake kama enzi zake akiwa
klabu ya Lille ya Ufaransa.
Mshambuliaji
huyo ndio wa mwisho kuondoka katika klabu ya Asernal muda huu wakati
kocha Arsene Wenger akisuka kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao wa ligi
kuu soka nchini England na ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Furaha ya mwisho: Msimu mgumu kwa Gervinho katika klabu ya Arsenal umefika tamati baada ya kukamilisha uhamisho kuelekea Roma.
Mapema
katika majira haya ya kiangazi, mchezaji mwenye rekodi ya kusajiliwa
kwa dau kubwa na Arsenal, Andrey Arshavin alitimka zake baada ya
mkataba wake kumalizika na wakati huo huo wachezaji Denilson, Sebastien
Squillaci, na Marouane Chamakh wanatarajia kufuata nyuma yake kutimka
Emirates majira haya ya joto.
‘Nimefurahia
kumsajili Gervinho kama nilivyofurahi baada ya kuwapata Morgan De
Sanctis na Kevin Strootman, Alisema kocha wa Roma, Garcia.
‘Gervinho
ni mchezaji wa haraka na kasi, anaweza kushambulia na ni mchezaji
mwenye aina ya pekee ya mpira ukilinganisha na wachezaji wengine.’
Kaenda zake Serie A : Gervinho anatarajia kufanya kazi na Rudi Garcia, kocha wake wa zamani akiwa Lille
Ana kipaji kikubwa: Lakini Gervinho hajapata nafasi ya kuonesha ubora wake katika dimba la Emirates
No comments:
Post a Comment