Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, August 9, 2013

HII NDO FASHION MPYA KWA WASANII WETU SASA....LINAH NAE ANAKUJA NA KIPINDI KIPYA CHA TV,NDANI YA CLOUDS TV

Linah Sanga anatarajia kuonekana kwa mara ya kwanza kwenye kipindi chake cha TV kiitwacho 3D kupitia Clouds TV.
Linah
Akiongea na Bongo5, Linah amesema show hiyo ya watoto itaanza kuoneshwa Jumapili hii. 3D itakuwa ikizunguka mitaani kuzungumza na watoto wenye vipaji mbalimbali vinavyostahili
kuendelezwa huku pia akiwasisitiza kusoma.
“Lengo langu ni kuwahamasisha wazazi kwa pande zote mbili kwamba wasiwalemaze watoto wao kwenye vipaji zaidi kuliko kwenye kusoma na kwa upande mwingine waheshimu vipaji ambavyo watoto wao wanavyo,” amesema.

No comments:

Post a Comment