Juma
Mgunda kulia akiongea jambo na Hussein Ngurungu mara baada ya mazishi
ya mdogo wake Idrisa Ngurungu aliyefariki kwa ajali ya gari katika barabara
kuu Morogoro-Kisaki eneo la Kibungo siku ya ijumaa Agosti 2 mwaka huu
mkoani Morogoro na kusababisha watu wawili kufariki dunia papo hapo na
wengine wanee kujeruhiwa vibaya katika ajali hiyo iliyotokea majira kati
ya saa 6 na saa 7 mchana mkoani Morogoro.
Jeneza lenye mwili wa mchezaji nyota
wa zamani aliyewahi kuzichezea klabu za Reli ya Morogoro, Pan Afrika ya
Dar es salaam na Coastal Union ya Tanga, ldrisa Ngurungu kulia na la
Laila Mgoto yakiwa katika makaburi ya Kola muda mfupi kabla ya mazishi
yao baada ya kuf
ariki dunia katika ajali ya gari barabara kuu
Morogoro-Kisaki eneo la Kibunge siku ya ijumaa agosti 2 mwaka huu mkoani
Morogoro.Jeneza lenye mwili wa mchezaji nyota
wa zamani aliyewahi kuzichezea klabu za Reli ya Morogoro, Pan Afrika ya
Dar es salaam na Coastal Union ya Tanga, ldrisa Ngurungu kulia na la
Laila Mgoto yakiwa katika makaburi ya Kola muda mfupi kabla ya mazishi
yao baada ya kufariki dunia katika ajali ya gari barabara kuu
Morogoro-Kisaki eneo la Kibunge siku ya ijumaa Agosti 2 mwaka huu mkoani
Morogoro.
Huyu
ni mchezaji wa zamani wa klabu ya Pan Afrika na Yanga Baakari Malima
(Jembe Ulaya) katika mazishia hayo ambapo Malima aliwahi kucheza na
Idrisa Ngurungu katika klabu ya Pan Afrika miaka hiyo.
Kocha John Simkoko naye akizungumza jamba na mmoja watu walioshiriki katika mazishi hayo.
Jeneza
la dada yetu mpendwa Laila Mgoto likiingizwa katika gari mara baada ya
sala ya mwisho katika msikiti wa Mjipya tayari kwa kuanza safari ya
kuelekea katika makaburi ya Kola kwa mazishi.
Sehemu
ya usafiri wa pikipiki waliotumia watu mbalimbali kuwasafirisha kutoka
nyumbani kwa marehemu hadi makaburi ya Kola kwa ajili ya kushiriki
mazishi hayo.
Magari yakielekea Kola katika mazishi hayo eneo la Kilima kwa Mnyonge Kilakala.
Kutoka
kulia ni marehemu Idrisa Ngurungu, Shomari Kapombe, Profesa Madundo
Mtambo na Hamis Machupa mara baada ya kumalizika kwa mazoezi hivi
karibuni katika uwanja wa Morogoro Veteran uliopo jirani na hospotali
kuu ya mkoa wa Morogoro. PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Na Juma Mtanda, Morogoro.
MCHEZAJI
nyota wa zamani aliyewahi kuzichezea klabu za Reli ya Morogoro, Pan
Afrika ya Dar es salaam, Coastal Union ya Tanga na timu ya taifa ya (Taifa Stars), ldrisa Ngurungu
amefariki dunia kwa ajali ya gari wakati akisafari kutoka Morogoro mjini
kwenda kijiji cha Kisaki kwa kuhudhuria mazishi ya mkwe wa
mdogo wake katika tukio lililotokea Agosti 2 mwaka huu majira kati ya saa 6 na saa 7 mchana mkoani Morogoro.
Akizungumza
na gazeti hili jana (juzi) wakati wa mazishi ya mchezaaji huyu katika
makaburi ya Kola mjini hapa, Shemeji wa marehemu, Nasibu Nasour alisema
kuwa Idrisa Ngurungu amefariki dunia baada ya kutokea ajali ya gari siku
ya Ijumaa katika barabara kuu Morogoro-Kisaki eneo la Kibungo wakati
wanafamilia wakielekea katika mazishi kijiji cha Kisaki na
kufariki dunia akiwa yeye na Laila Mgoto papo hapo na abiria wengine wanne
kujeruhiwa vibaya.
Nasour alisema kuwa
mazishi ya ndugu zao Idrisa Ngurungu pamoja na Laila Mgoto wamezikwa
katika makaburi ya Kola na katika ajali hiyo ndugu wengine wanne walijeruhiwa na kulazwa katika
hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro baada ya dereva aliyekuwa akienda gari hilo, Moshi
Gimbi kujaribu kuepusha ajali ambayo ingeweza kutokea na gari nyingine ya kugongana uso kwa uso katika
kona eneo hilo la Kibungo na kupinduka huku ikisababisha watu wawili
kufariki dunia papo hapo abiria wanne wakijeruhiwa ambapo
Ngurungu na mpwa wake Laila Goto wamezikwa katika makaburi ya Kola majira
ya saa 10 jioni.
Mazishi hayo yalihudhudliwa na viongozi
mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Innocent
Kalogeris, Meya wa Manispaa ya Morogoro Amiri Nondo, Mbunge wa Morogoro
mjini Abdullaziz Abood pamoja na wachezaji wa zamani wa klabu za Coast
Union wakiongizwa na Mwenyekiti wa Coast Union, Ahmed Hilal, Saidi Korongo, Juma Mgunda, Dogras Muhani, Razack Yusuph,
Bakari Malima (Jembe Ulaya) huku wachezaji wa Reli Morogoro wakiongizwa
na Kocha John Simkoko, Peter Mjata, Boniface Njohole na Mohamed Mtono.
Aliwata
ndugu waliojeruhiwa katika ajali hiyo na kulazwa hospitali ya mkoa wa
Morogoro kuwa ni pamoja na Salum Kapilima, Abushir Moto, Halima Muya na
Bahati Seif ambao wameumia sehemu mbalimbali za miili yao.
“Tulikuwa
tunakwenda kumzika (Yakubu Ngurungu) ambaye ni mkwe wa mdogo wake
marehemu Idrisa katika mji mdogo wa Kisaki aliyefariki dunia siku mbili
kabla ya tukio hilo, na gari lao lilichelewa kuondoka mjini ambapo mimi
na wanafamilia wengine tulitangulia na gari walipofika eneo la Kibunge
lilipinduka na watu wawili wafariki dunia papo hapo na wanne
wakijeruhiwa vibaya na ajali hiyo ilitokea kwa sababu ya mwendo kasi
uliochangia na dereva kutoifamu kona za barabara hiyo”. Alisema Nasour.
Naye
mchezaji mwenzake wa zamani wa klabu ya Reli ya Morogoro Hamis Machupa
alisema kuwa kifo hicho kimewastua wengi wakiwemo ndugu, jamaa na
marafiki kutokana na mazingira ya tukio hilo kwani siku ya alhamisi
yeye, Bure Mtagwa na marehemu Idrisa Ngurungu aliomba fedha kwa (yeye
Hamis Machupa) kwa ajili ya kumsaidia katika safari ya kwenda Kisaki
katika mazishi ya mkwe wa mdogo wake (Yakubu Ngurungu) aliyefariki dunia
hivi karibuni na mazishi yake kufanyika Kisaki.
Machupa
alisema kuwa alionana na marehemu siku ya alhamisi baada ya kutoka
mazoezini uwanja wa Morogoro Veterani na walifika nyumbani kwao Idrisa
Ngurungu kumpa pole na kutoa kiasi cha fedha kisha kuagana naye ambapo
marehemu alieleza kuwa baada ya mazishi angeweza kurudi siku hiyo hiyo
(kesho yake Ijumaa) lakini kufika majira ya saa 9 alasili siku ya Ijumaa
alipigiwa simu na kuelezwa taarifa za kifo cha Ngurungu. alisema
Machupa.
No comments:
Post a Comment